MASHINDANO ya kombe Mbuzi Cup yatafikia tamati
tarehe 30 mwezi wa tatu kwa kuzikutanisha timu za Mkwawa Rangers na Waandishi
wa habari mkoa wa Iringa na fainal hiyo itachezwa katika kijiji cha Kalenga
kata ya Kalenga wilayani Iringa mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua vipaji wa
wachezaji kata hiyo.
Akishudia mchezo wa nusu fainal kati ya timu ya Waandishi wa habari mkoa
wa Iringa (IMFC) na timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa
kalenga katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa
mgeni rasmi alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani
kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania
wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa
sasa,
"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu
kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya
taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Chitinka
Aidha Chitinka aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa
miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya
ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini
hata nje ya nchi.
“Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua
vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu mbalimbali na lengo likiwa ni
kuhakikisha vipaji vyote vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni
ajira si mnamuana mchezaji Mbwana Samatta”.alisema Chitinka
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Obeid
Msigwa aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya
bora ambayo itakuwa ikiwakilisha katika mashindano ya mbalimbali.
“Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na
viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na
mishahara wanayopata”, alisema Msigwa
Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo kamanda wa
vijana wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya Iringa Jackson Kiswaga alisema
ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa
wilaya ya Iringa.
“Ilani ya chama cha mapinduzi inatutaka mwenyeviti
kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa
taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema Kiswaga.
Mashindano ya Mbuzi Cup ni miongoni mwa mashindano
yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya
kucheza katika vilabu vikubwa nchini.
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwasalimia
wachezaji wa timu ya Waandishi
wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu
ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano
ya Mbuzi Cup.
No comments:
Post a Comment