Kampuni
ya Kimataifa ya Uhandisi katika utengenezaji wa vyombo vya Moto ya Mahindra
yenye Makao Makuu yake Mjini New Delhi Nchini India imeamua kuiunga Mkono
Zanzibar katika muelekeo wake wa kuimarisha miradi ya maendelelo.
Mkuu
wa shughuli za Kimataifa wa Kampuni hiyo Bwana Arvind Mathew alitoa kauli hiyo
wakati wa kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni yake na Ujumbe wa
Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
kilichofanyika Makao Makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Mjini New Delhi.
Bwana
Arvind Mathew alisema kutokana na kukuwa kwa Teknolojia ndani ya Kamupuni ya
Mahindra, Uongozi wa Taasisi hiyo ya Uhandisi Nchini India hivi sasa umekusudia
kuelekeza nguvu zake katika Mataifa rafiki kwa nia thabiti ya kuona Mataifa
hayo hasa yale ya Bara la Afrika yanakuwa Kiuchumi.
Alisema
Mahindra imejipanga kuangalia njia za kusaidia uimarishaji wa Sekta ya Kilimo
kupitia miundombinu imara na vifaa vya Kisasa vitakavyoongeza nguvu za
uzalishaji kwa kundi kubwa la Wakulima katika mazao ya viungo yenye tija kubwa
katika soko la Kitaifa na Kimataifa.
Alisema
Wataalamu wa Kampuni ya Mahindra wamekuwa shahidi katika safari zao za kawaida
kwenye Mataifa mbali mbali waliyowekeza miradi yao ya Kiuchumi kuwaona Wakulima
wa maeneo hayo wakiendesha shughuli zao katika mazingira magumu.
Bwana
Arvind Mathew alieleza kwamba wakulima wengi hasa katika Nchi changa
zinazojikita kuendelea wamekosa Taaluma ya kutosha katika kuimarisha Kilimo
chao jambo ambalo wanadiriki kupata kipato kidogo huku wakitumia nguvu nyingi
zaidi wakati wa uzalishaji.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara cha Kampuni ya Mahindra Kanda ya
Afrika Bwana Saurabh Kohli aliueleza Ujumbe wa Zanzibar ulio mwishoni mwa ziara
yake Nchini India kwamba Mahindra imekusudia kuwa na Mtandao wa Kimataifa
katika mfumo wa Uzalishaji katika Nchi mbali mbali walizowekeza Ulimwenguni.
Bwana
Saurabh Kohli alisema Mahindra iliyoasisiwa kwama 1945 ikianza na uzalishaji wa
gari aina ya Jeep kwa sasa tayari imeshawekeza katika Mataifa Mia Moja kwenye
nchi mbali mbali Duniani ikiwa na wafanyakazi wasiopungua Laki 200,000 ikianza
na mtaji wa Dola za Kimarekani U$ Bilioni 16.5.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya ujumbe wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Seif
alisema ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Zanzibar na Kampuni ya Mahindra
umetoa mchango mkubwa katika kuwakomboa Wananchi na hasa Wakulima wa Zanzibar.
Alisema
Wananhi wa Zanzibar zaidi ya asilimia 70 walioko Vijijini katika Visiwa vya
Unguja na Pemba wanaendesha maisha yao ya kila siku kwa kutegemea sekta ya
Kilimo. Wakati huo huo Ujumbe wa Zanzibar ulikutana kwa mazungumzo na
Wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara tofauti wa Mji wa New Delhi na Majimbo
jirani yanayouzunguuka Mji huo yaliyofanyika Makamo Makuu ya Shirikisho la
Viwanda la India { CII }.
Katika
mazungumao yao Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo ambae pia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K Kapila alisema India
na Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa ujumla zimekuwa na ushirikiano wa karibu wa
Kibiashara uliotiwa saini mnamo mwaka 1974.
Bwana
Kapila alisema ushirikikano huo unaoendelea kuimarika kila siku umeibuwa
mchango mkubwa wa msaada wa fedha zitakazosaidia uimarishaji wa huduma za Maji
safi na salama katika Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar kufuatia ziara ya mwaka
jana ya Uongozi wa ngazi ya juu ya India uliofika Tanzania Mwezi Disemba mwaka
2015.
Uwepo
wa wafanyakazi zaidi ya 10,000 wanaotoka Nchini India wakifanya kazi Tanzania
na Zanzibar kwa ujumla ni uthibitisho wa ushirikiano uliopo kati ya pande hizo
mbili.
Naye
kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Zanzibar
imeshafungua milango ya uwekezaji kwa makampuni mbali mbali ndani na nje ya
Nchini tokea miaka ya 90.
Alisema
zipo sekta ambazo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshazijengea uwezo kwenye
miundombinu itakayotoa wepesi kwa Taasisi pamoja na Makampuni yenye nia na
maamuzi ya kutaka kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi Visiwani Zanziobar.
Balozi
Seif aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa inapatikana katika sekta ya Afya,
Kilimo, Miundombinu, Elimu pamoja na sekta isiyo ya kiserikali inayotoa ajira
kubwa zaidi kwa makundi ya akina mama na Vijana.
No comments:
Post a Comment