MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia
mbali maombi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka asikamatwe hadi kesi yake ya
kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda itakapomalizika.
Maombi hayo yalitupwa kwa
sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua si sahihi na kwamba hutumika
pale ambapo sheria ziko kimya.
Uamuzi huo wa majaji
umefikiwa kutokana na pingamizi la jamhuri lililowasilishwa na Wakili wa
Serikali Mkuu Gabriel Malata kuiomba kuyatupilia mbali maombi hayo kwani hayana
msingi kisheria.
Katika hatua nyingine,
mwanahabari nguli nchini Jenerali Ulimwengu, ameungana na jopo la mawakili
Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Malya katika kumtetea Mbowe.
Mbowe amefungua kesi hiyo
ya kikatiba namba 1, ya mwaka 2017 dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar
es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi 8, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akitafakari jambo ndani ya Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam akiwa na wakili wake Jenarali Ulimwengu (kati), na Meya wa Ubungo Boniface Jacob .
No comments:
Post a Comment