WATU watatu raia wa Nchi ya Burundi waliopewa hifadhi katika Kambi ya
wakimbizi ya Mtendeli Mkoa wa Kigoma, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi la hapo, kwa
tuhuma za upangaji wa magogo katika barabara kuu ya Kigoma, Kasulu na Kakonko
kwa lengo la utekaji wa magari hasa mabasi ya abiria yaendayo mikoani.
Pia, walipokaguliwa walikutwa na vitu vifuatavyo Bomu moja la kutupwa
kwa mkono (Offensive hand Grenade), Bunduki moja ya bandia, panga mbili, rungu
3, viatu aina ya raba jozi moja, viatu vya kike jozi moja, simu aina ya nokia
Nne, Tecno tatu, vipodozi vya kike, laptop, power benki, saa, sanjari na nguo
mbalimbali za kiume.
Akizungumzia tukio hilo leo mbele ya wandishi wa habari ofisini kwake
kigoma Ujiji, Kamanda wa Polisi Ferdinand Mtui alisema walibaini hilo baada ya
askari polisi waliokuwa katika doria kwenye njia hiyo yenye mapori makubwa
ndipo waliwakamata watuhumiwa hao ambao walikuwa kwenye mtego.
Aliyataja majina ya watuhumiwa hao ni pamoja na Hakizimana David (21), Nepomseni
Niogere (25) na Nduwamahoro Justine (20) wote ni wakimbizi wanaoishi katika
kambi ya mtendeli iliyopo wilaya ya Kakonko na watafikishwa mahakamani baada ya
uchunguzi kukamilika.
Alitoa mwito kwa raia wote wa kigeni waliopewa hifadhi katika kambi
mbalimbali za wakimbizi mkoani humo watii sheria, kanuni na taratibu zote za
nchi na waache kujihusisha na vitendo
No comments:
Post a Comment