Kikao cha siku tano cha wabobezi/wataalamu katika
mambo ya miliki bunifu, kinaendelea kufanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano
katika Shirika la Utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Msasani
jijini Dar es Salaam, ambapo kikao hicho kimejumuisha Wadau kutoka Serikalini
sambamba na Sekta binafsi.
Mchakato wa kikao hicho unafuatia wakati shirikisho
la filamu Tanzania (TAFF) lilipoanza kufanya mchakato wa tatifi ya sera ya
miliki bunifu tangu miaka minne iliyopita kwa kufadhiliwa na wahisani
‘Best Dialogue’, ambapo mwaka 2013 inaelezwa kuwa tafiti hiyo ndio ilipelekwa
rasmi Wizarani kwa ajili ya kuendelea na mchakato zaidi.
Rais wa Shirikisho la Filamu hapa nchini (TAFF),Simon Mwakifwamba, alisema
kuwa Mkutano huo wa kuhitimisha rasimu ya sera ya miliki bunifu, ni sera ambayo
ilipatikana kwa kufuata taratibu zote, kwa maana ya ushirikishwaji kwa upande
wa serikali na Sekta binafsi, Mwakifwamba alisema kwa upande wao kama wasanii
hiyo ndio sehemu yenyewe muhimu ambayo wasanii wamekuwa wakiiliia kwa muda
mrefu.
"Kwa mchakato huu sisi kama wadau tunasema
kwamba hapa tulipofika tuko pazuri, na nina imani na wataalamu hawa kwamba
tukiwa na juhudi za pamoja tutaweza kuhitmisha hii rasimu hii ya
miliki bunifu na mwisho wake tutatoka na sera nzuri, na kama tutakuwa na
msingi mzuri wa kuwa na sera nzuri itatupelekea na kuwa na sheria nzuri, tukiwa
na sheria nzuri tutakuwa na kanuni nzuri, tukiwa na vitu hivyo vitatu tunaamini
serikali itakuwa imetengeneza mazingira mazuri kwa wabunifu wote katika Nyanja mbalimbali,
kwamba hii sera itakuwa yenye tija na mafanikio makubwa kwa nchi na hata
kwetu wasanii kwa ujumla" alisema Mwakifwamba.
Kaimu Mkurugenzi
Msaidizi Biashara ya nje, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wilson
Malosha akizungumza mbele ya wanahabari na Wadau mbalimbali katika kikao
cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu, kilichofanyika
jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta
binafsi, Kulia ni Rais Shirikisho la Filamu hapa nchini, Simon Mwakifwamba.
Wadau mbalimbali
wakifutilia yaliyokuwa yakizungumzwa kutoka meza kuu, katika kikao cha siku
tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu, kilichofanyika
jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini
yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa
rasimu ya sera ya miliki bunifu, kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na
baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi.
No comments:
Post a Comment