Benki ya NMB imemwakikishia Rais wa Tanzania, Dkt.
John Magufuli kuwa itaendelea kutumia mifumo ya kiteknolojia ili kuwawezesha
wateja wa benki hiyo kutumia Zaidi mifumo ya kietroniki kuliko unaotumika Zaidi
kwa sasa wa malipo kwa kutumia pesa taslim.
Hayo ya mesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke
Bussemaker wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Kibiashara cha Mtwara na kueleza
kuwa nia ya benki ni kuendelea kukua Zaidi huku ikitoa suluhu ya vipau mbele
vya serikali na kujikita katika ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia
zakielektroniki.
“Kwa kutumia teknolijia mbalimbali, NMB tumewekeza
Zaidi kwenye kutatua changamoto mbalimbali za wateja wetu na hivyo kutoa fursa
za kutumia Zaidi njia za benki kuliko kutumia njia za malipo kwa kutumia pesa
taslim,” alisema Ineke.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
NMB, Prof. Joseph Semboja alisema kuwa NMB imefanya maboresho makubwa na hivyo
kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa huduma za kifedha kwa kila kada ya watanzania na
serikali kwa ujumla.
Prof. Semboja alisema kuwaSerikali kwa sasa
inamiliki hisa asilimia 32 ndani ya benki ya NMB zenye thamani ya Zaidi ya
Bilioni 430 hivyo kuiwezesha serikali kupata gawio la Zaidi ya bilioni 75 ndani
ya miaka mitano.
“Kwa mwaka huu mheshimiwa raisi, kama mkutano mkuu
wa wanahisa utakaokaa mwezi wa sita mwaka huu, utabariki Kiwango cha gawio,
serikali itapata gawio la shilingi Bilioni 16.5 zinazotokana na faida
iliyopatikana mwaka 2016,” alisema Prof. Semboja.
Nae Rais Magufuli aliwapongeza NMB kwa huduma
wanazotoa na kutoa wito kwa viongozi wa serikali na wakuu wa wilaya na viongozi
waliopo ndani ya serikali kufanya biashara na NMB kwani serikali ina hisa
kwenye benki hiyo na hupata faida kutoka NMB.
“Nikuombe Waziri, toa maelekezo kwa sababu wewe ndo
unasimamia pesa, pesa ya serikali ipitie NMB ili nipate gawio kubwa zaidi, wale
wengine wanaofanya biashara bila kuifaidisha serikali na kugawana gawio wao kwa
wao huku serikali haipati faida yoyote, hatutafanya biashara nao,”
alisemaRaisiMagufuli.
Rais Magufuli pia aliiomba NMB kushiriki katika
kuunga mkono ajenda ya serikali katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Rais Magufuli alisema kuwa,“Naomba NMB mshiriki
katika kukopesha viwanda hasa viwanda vidogovidogo na hivyo kuunga Mkono juhudi
za serikali katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.”
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker mara
baada kukifungua rasmi kituo cha Biashara cha NMB mjini Mtwara kijulikanac ho kama
Mtwara Business Centre. Pamoja na mambo mengine, rais magufuli alimuagiza
Waziri wa fedha Dr Philip Mpango kuhakikisha kuwa fedha zote za serikali
zinapita NMB.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli pamoja na Mkurgenzi wa NMB – Ineke Bussemaker wakikata utepe kuashiria
ufunguzi rasmi wa kituo cha kibiashara cha NMB – NMB Business Centre mjini
Mtwara juzi. Kutoka kulia niAfisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati – Abdulmajid
Nsekela, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi – Prof Joseph Semboja na kutoka
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara – Halima Dendegu na Waziri wa Fedha na
Uchumi – Dr
Philip Mpango.
No comments:
Post a Comment