STAA
wa sinema za Kibongo, Deogratius Shija amefunguka kuwa, wasanii wanamtenga,
kisa sakata la unga ambalo lilimsababishia kuwekwa sero bila kujua sababu ya
yeye kuingia huko.
Akizungumza
na Wor’Out Media baada ya kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam
alikowekwa sero kwa siku 15, Shija alisema katika sakata hilo ambalo lilihitaji
faraja ya wasanii wenzake, hakuna aliyemtembelea zaidi ya mwigizaji William
Mtitu aliyemfariji kwa kumpelekea maji na sabuni.
“Sasa
nimejua ndugu na rafiki wa kweli. Ninamshukuru Mtitu maana yeye tu ndiye
alijitolea kuniona bila kujali nimefanya au sijafanya,” alisema Shija.
Akisimulia
mkasa mzima wa kukamatwa kwake, Shija alisema kuwa, anakumbuka ilikuwa usiku wa
Februari 9, mwaka huu ambapo askari walifika nyumbani kwa rafiki wa Shija
aliyemtaja kwa jina moja la Liberty, wakiwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa
kisha kuwakamata.
Alisema
askari hao walisema kuwa walikuwa wakimsaka rafiki wa jamaa aitwaye Mwinyi
Machapta waliyemtaja kwa jina la Liberty. “Walipofika walituchukua hadi
‘Sentro’ wakatusweka ndani kwa siku 15.
Sikuhojiwa kwa lolote zaidi ya kujieleza na
baada ya hapo, walinirudisha sero wakanifungulia faili la uchunguzi, walichukua
simu lakini hadi leo siwezi kukuambia nimekosa nini ila nilikamatwa kwa sababu
ya rafiki yangu, Liberty kwani ninaishi naye,” alisema Shija.
No comments:
Post a Comment