Msafara wa mabingwa wa
watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC , umewasili salama jijini Dar
es salaam ukitokea Morogoro walipokwenda kucheza na Mtibwa Sugar kwa matokeo ya
sare ya 0-0.
Msafara huo umeelekea
moja kwa moja kambini kwa maandalizi ya michezo miwili muhimu itakayofanyika
kesho machi 7, 2017 dhidi ya Kiluvya United uwanja wa Taifa na machi 11, klabu
bingwa Afrika dhidi ya Zanaco FC.
Timu imeendelea na
mazoezi jioni ya leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kesho robo fainali
kombe la FA dhidi Kiluvya ya kutoka mkoani Pwani .
Kocha mkuu wa Yanga, George Lwandamiana amesema kuwa licha ya ratiba ngumu kuikabili timu yake
lakini amesema yupo tayari kupambana na vijana wake ili kuhakikisha klabu
inapata matokeo mazuri katika michezo yote miwili.
Wapenzi, wanachama,
mashabiki na wadau wa soka mnaombwa kujitokeza kwa wingi katika michezo yote
miwili ili kuipa sapoti timu hiyo .
Mbali na hilo, droo ya kombe la Shirikisho hatua ya saba au robo
fainali inatarajiwa kufanyika kesho baada ya kupatikana kwa mshindi wa
mechi kati ya Yanga na Kiluvya na kuungana na timu za Simba na Azam FC za
Dar es Salaam, Mbao FC ya Mwanza, Tanzania Prisons ya Mbeya, Madini ya Arusha,
Kagera Sugar ya Bukoba na Ndanda FC ya Mtwara.
No comments:
Post a Comment