Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel (wa nne kutoka kushoto) na Naibu
Waziri wa Masuala ya Utangazaji, Filamu na Habari wa China, Tong Gong
(katikati), wakikata utepe kuzindua maonyesho ya kwanza ya tamthiliya ya China
ya 'Mfalme Kima' iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Uzinduzi huo umefanyika
leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Jiang Almin, ambaye ni
Mkurgenzi wa Radio China Kimataifa, wa pili kutoka kulia ni Suzan Mungy
(Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma na Matukio wa Shirika la Utangazaji Tanzania -
TBC) na wa nne kulia ni Ma Li (Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Kimataifa
wa China).
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel, akizungumza wakati wa uzinduzi wa
maonyesho ya kwanza ya tamthiliya ya China ya 'Mfalme Kima' iliyotafsiriwa kwa
lugha ya Kiswahili.
Ma Li, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya
Kimataifa wa China, akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo hii jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa StarTimes, Guo Zingi,
akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthiliya ya 'Mfalme Kima' ambayo ni ya
Kichina iliyotafsiriwa kwa Kiswahili.
Suzana Mungy, Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma na
Matukio wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akizungumza wakati wa uzinduzi
wa tamthiliya ya Kichina ya 'Mfalme Kima' iliyotafsiriwa Kiswahili. Uzinduzi
huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurgenzi wa Radio China Kimataifa, Jiang Almin, akizungumza
wakati wa uzinduzi huo.
Meza kuu ya wageni wa heshima katika uzinduzi huo.
Akinadada wa StarTimes wakiwa wamejiandaa kabla ya kukatwa kwa utepe kuashiria uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya China ya Mfalme Kima iliyotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili.
Wageni waalikwa wakifuatilia mambo yaliyokuwa yakiendelea.
Wasanii wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo.
Wageni
mbalimbali wakifuatilia.
Picha ya pamoja ya
wafanyakazi wa StarTimes, wasanii wa wageni wa heshima.
Na Hassani Makero
SERIKALI ya China kupitia Wizara ya Utamaduni ya nchi
hiyo imeombwa kutangaza filamu za Tanzania nchini humo ili kuutangaza utamaduni
wa Watanzania.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo hii na
Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma na Matukio wa Shirika la Utangazaji Tanzania
(TBC), Suzana Mungy, wakati akitoa hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBC
katika hafla ya uzinduzi wa maonesho ya kwanza ya Tamthiliya ya China ya
(Mfalme Kima) ya lugha ya Kiswahili uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam leo.
"Ni vema sasa na wenzetu wa China wakawa
wanaonesha filamu zetu huko kwao kwa lugha ya Kichina ili kusaidia kutangaza
utamaduni wetu," alisema Mungy.
Mungy alisema Wachina wamekuwa wakionesha filamu zao
hapa nchini ambazo zimeingizwa sauti kwa lugha ya Kiswahili na Watanzania hivyo
ili kupanua wigo wa mahusiano katika tasnia hiyo ni vema pande zote mbili
zishirikiane kuandaa tamthiliya ya pamoja ya lugha ya Kiswahili.
Mkurugenzi Mtendaji wa StarTimes, Guo Zingi, alisema
kwamba kampuni yake imejizolea mashabiki wengi nchini Tanzania kutokana na
kuonesha filamu na tamthiliya nyingi za Kichina zilizotafsiriwa Kiswahili,
lugha ambayo inaeleweka.
Alitolea mfano tamthiliya ya Maudodo, kama mojawapo ya
tamthiliya hizo ambayo ilijizolea umaarufu kwa watu wa rika zote nchini
Tanzania.
Aidha, amekiri kwamba, kwa sasa ziko tamthiliya na
filamu nyingi za Kichina zinazotazamwa nchini Tanzania ambazo zimetafsiriwa
Kiswahili.
Alisema mapema mwaka 2016 kampuni hiyo ilifanya
mashindano ya kuwapata vijana 10 wa Kitanzania waliopelekwa China kwa lengo la
kwenda kuingiza sauti za Kiswahili katika filamu na tamthiliya mbalimbali za
Kichina, hatua ambayo imesaidia kuzifanya tamthiliya hizo zipendwe na
kukubalika nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Masuala ya Utangazaji, Filamu na
Habari wa China, Tong Gong, alisema uhusiano huo baina ya Tanzania na China
utaendelea kudumishwa katika masuala ya utamaduni kama iliyo katika maeneo
mengine maendeleo.
Kupitia tamthiliya mbalimbali, watakuwa wakibadilisha
utamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni
na Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel, alisema Tanzania na China wataendelea
kushirikiana na kudumisha uhusiano ulioasisiwa na waasisi wa mataifa hayo -
Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tsetung.
"Kwa kuwa wenzetu China mko juu katika teknolojia
ya utangazaji na mawasiliano, ninawaomba muangalie namna ya kuisaidia Tanzania
katika tasnia ya sanaa na utamaduni ili na wasanii wetu nao kazi zao ziweze
kupata masoko huko," alisema Profesa Ole Gabriel.
No comments:
Post a Comment