TUMIA KALENDA YA UTE KUKWEPA MIMBA ZISIZOTARAJIWA NA KUPANGA MTOTO UMTAKAE - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, March 25, 2017

TUMIA KALENDA YA UTE KUKWEPA MIMBA ZISIZOTARAJIWA NA KUPANGA MTOTO UMTAKAE




Kama mzunguko wa mwanamke ni kigeugeu yaani mwezi huu 28 mara 30 au 32 ama unaenda siku tatu, nne, tano au hata sita kwa vipindi tofauti, basi itakuwa vigumu kwa mwanamke kukwepa kupata mimba kwa kusoma kalenda.

Njia sahihi ni ya kusoma ute (kipindi cha joto). Ndiyo maana wanyama kama ng'ombe, mbuzi na wengineo, kila wanapojamiana kinachofuata huwa ni mimba tu, wao hutumia kalenda ya ute wa uzazi.

Kwa mwanadamu kuna aina tatu za ute muhimu, zikizidi tatu yaweza kukawa na maambukizi.
Ute Wa kwanza ni ute mweupe mzito, huu sio ute wa uzazi kwa kipindi chochote utakapo onekana. Kwani unazuia mbegu za baba kulifikia yai. Ute huu huua mbegu za baba ndani ya dakika 30 hivyo aina hii ya ute haina uzazi.

Ute mwepesi, huu ni ute ambao tunauita "subiri kidogo" maana yawezekana ukawa umetokana na mihangaiko ya mama kukasirika, kuchoshwa, kuumwa homa au ikawa ni dalili ya yai kukomaa. Hivyo ukiuona ute huu subiri siku moja uone kama ute utakata au kuongezeka.

Iwapo ute huu utaendelea kwa Siku mbili hadi tatu jua hapo kuna uzazi. Lakini atakaye tungwa ni mtoto Wa kike. Hivyo kama lengo ni kukwepa mimba usifanye tendo la ndoa.

Iwapo utapenda mtoto Wa kiume; Subiri kuanzia hapo kwenye ute mwepesi mpaka "ute unaoteleza kama kiini cha yai". Ute huu una uzazi asilimia 98 na unalenga kutungisha mtoto Wa kiume asilimia 99.

Hivyo basi kama wewe siku zako hazigandi, jifunze kalenda ya ute na itakusaidia kupata mimba kwa kila tendo la ndoa utakalolifanya. Na itakusaidia kuchagua ni mtoto wa aina gani unamuhitaji.

Kadhalika itakusaidia kukwepa mimba usiyoihitaji. Kalenda ya mzunguko wa tarehe wengi wameshindwa kuitambua vyema kwa sababu ya kubadilika badilika kwa siku zao zao hedhi kutokana na mikikimikiki ya maisha ambapo iwapo mama atasafiri safari ndefu tu bila kujali umbali wa safari, siku zake za hedhi zinaweza kuongezeka au kupungua.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages