Jumuiya
ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki
mjini Northampton, katikati ya Uingereza jumamosi ya tarehe 1 April 2017.
Tafrija
hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na marafiki zao
wa Kenya, Uganda, Kongo, Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na Mheshimiwa
Balozi Dk Asha Rose Migiro.
WASATU ilibuniwa mwaka jana
kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na
promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya. Asilimia 20 ya kipato cha
onesho zilitolewa na WASATU kwa waliofikwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni
Tanzania.
Watanzania
na marafiki zao wakijimwaga ukumbi wa The Eastern District Social Club,
Northampton.
Furaha
na shangwe ya WASATU
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk Asha Rose
Migiro (katikati) na mwana WASATU - Mcheza ngoma asilia, Khadija Ismail. Wa
kwanza ni Mtanzania, Salma Kashinde
Muziki motomoto, Northampton
Bango
la shughuli hiyo lilikuwa hivi
Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza Dk Asha Rose Migiro akihutubia tafrija hiyo
Mpiga
saksafoni mkongwe na mwanaWASATU- RamaSax- mzawa wa Tanga akipuliza vituz
WASATU:
Toka kushoto nyuma, Rama Sax, Saidi Kanda, John Londo, Fab Moses , Freddy Macha
Mbele : Khadija Ismail na Neema Kitilya.
Vitumbua vya Neema Kitilya
Nyama
Choma
Mwana
WASATU Fab Moses akionesha vituko vyake vya Sarakasi
Mwanamuziki mlemavu na msanifu picha, Kea , toka
Kenya aliyetengeneza tangazo la WASATU
Mwanamuziki
wa Kikongo Mboka Lia (anayejulikana kwa jina “Burkina Faso”) ndani ya nyuzi na
sakata sakata la WASATU
Mwanamuziki
mlemavu aliyekomaa - mtunzi, mwimbaji na mpiga gitaa hatari, John Londo – mwana
WASATU aliyebobea. Kileleni Northampton bila kukosa.
No comments:
Post a Comment