KLABU ya Soka ya Kagera
imeiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kulalamikia maamuzi
yaliyotolewa na kamati ya saa 72 kwa kuipatia pointi tatu timu ya Simba
ikidaiwa wamemchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.
Barua hiyo iliyopelekwa
moja kwa moja kwa Mtendaji Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa imeandikwa na
Mwenyekiti wa klabu hiyo Hamis Mdaki na kuelekeza malalamiko yao ya
kutokubaliana na maamuzi ya kamati ya saa 72.
Hukumu ya kuipatia Simba
alama hizo ilitoka juzi usiku baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Mohamed Yahya
alitoa maamuzii hayo mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa kamati
imethibitisha kuwa Mchezaji Mohamed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano
alizozipata katika michezo dhidi ya Prisons, Majimaji na African Lyon.
Hukumu hiyo imeonekana
kutokukubalika kwani kamati ilishindwa kupitia ripoti za waamuzi baada ya
kuonekana kutofautiana baina ya mwamuzi na kamisaa wa mchezo na kuamua kuwaita
waamuzi waje kuthibitisha kama ni kweli Fakhi alipewa kadi ya njano.
Kagera wamemtaka katibu
mkuu kuiangalia upya hukumu hiyo kwani wana uhakika kuwa Fakhi alikuwa na kadi
mbili za njano na sio tatu kama wanazodai Simba. Katika mchezo huo wa Kagera
walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Simba uliochezwa kwenye
dimba la Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.
Baaada ya maamuzi hayo
Simba wamejikita kileleni zaidi wakiwa na alama 61 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 56.
No comments:
Post a Comment