Kikosi cha wawakilishi
watanzania katika michuano ya kimataifa ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Yanga wamewasili salama nchini Algerai kwa ajili ya mchezo wao marudiano dhidi
ya MC Alger utakaochezwa kesho majira ya saa 2 usiku kwa saa za Afrika
Mashariki.
Katika msafara huo
uliiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa umefika salama na
ukipokelewa na watanzania wanaoishi nchi Algeria na kufurahishwa na mapokezi
hayo na kuahidi ushindi kwa watanzania.
Msafara wa wachezaji hao
uliingia kwa mafungu mawili ambapo kundi la kwanza liliwasili likiongozwa na
benchi la ufundi la timu hiyo likiwa na kocha Mkuu George Lwandamina huku kundi
la pili likiwasili na Katibu Mkuu.
Mtanzania Hamis Mwampese
anayeishi nchini Algeria amesema kuwa timu ya Algers wameingia uoga hasa baada
ya kuona Yanga wamechelewa kuingia nchini humo na zaidi kwa kufanya hivyo
wameepusha sana kufanyiwa hujuma na wenyeji wa nchi hiyo.
Yanga wamefikia katika
Hotel ya nyota tano inayojulikana kwa jina la Sultan ambapo si mbali sana na
Uwanja ulipo utakaochezewa kesho katika mechi hiyo ya marudiano ambapo Yanga
wanatakiwa kupata ushindi wa aina yoyote au sare.
Mtanzania
Hamis Mwampese akisalimiana na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa baada ya
kuwasili Jijini Algeria kwa ajili ya mechi ya marudiano ya hatua ya
mtaoano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Mc Alger ambapo katika
mechi ya awali Yanga walitoka na ushindi wa goli 1-0.
Mtanzania Hamis Mwampese akiwa katika picha
mbalimbali na wachezaji wa timu hiyo baada ya kuwasili nchini Algeria kwa ajili
ya mechi ya marudiano ya hatua ya mtaoano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika
dhidi ya Mc Alger ambapo katika mechi ya awali Yanga walitoka na ushindi wa
goli 1-0.
No comments:
Post a Comment