Ni miezi mitano sasa tangu
kuanza kwa ujenzi huu. Kuaza kwa ujenzi huu ni moja ya juhudi zinazo fanywa na
Serikali ya awamu ya tano, katika hili Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda amesema Rais pia hapa ataweka jiwe la msingi.
"Wazee wetu
waliteseka na familia zao kulikuwa na mgogoro mkubwa katika eneo hili kwa
kuwa Rais ni msikivu alisikia kilio cha wananchi wake na kumaliza
matatizo yao. Rais Magufuli akiahidi anatimiza na akisema ana maanisha
naombeni wanachi wote tumuunge mkono".
Kwa mujibu wa mratibu wa
ujenzi huu Christina Shayo eneo hili lina jengwa nyumba za ghorofa, majengo
matano yatakuwa na ghorofa 8 na apartment 656,
Gharama ya ujenzi huu ni
Bilioni 20 na unatarajiwa kukamilika kwa muda wa mwaka mmoja na ambapo
tayari miezi mitano inaelekea kuisha tangu ujenzi kuanza.
Kwa upande wake Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sita amesema maamuzi yaliyo
fanywa na Rais Magufuli kumaliza mgogoro wa eneo hili na kuanza kwa
ujenzi kumesaidia sana wananchi kwa kuwa waliteseka kwa muda mrefu na
kumepunguza malalamiko kwa ofisi ya Meya ambapo mwanzo watu walikuwa wanaenda
ofisi hiyo kulalamika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akiwasili eneo la ujenzi wa
nyumba za makazi ya wananchi katika eneo la Magomeni quotors (Kota)
akiambatana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta,
mapema jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akikaribishwa na waratibu
wa ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akitaka maelezo ya
maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi katika eneo la Magomeni
quotors (Kota) kutoka kwa waratibu wa ujenzi huo kutoka TBA.
RC Makonda wakwanza kushoto akipata melezo mafupi kutoka kwa wataalam
waujenzi akiwa ameambatana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin
Sitta aliyeko katikati watatu kutoka kushoto wakwanza kutoka upande wa
kulia ni mratibu wa ujenzi katika eneo hilo Arch Christina Shayo wa TBA.
Mratibu wa ujenzi katika eneo hilo Arch Christina Shayo wa TBA,
akitoa maelekezo kuhusu ujenzi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda
alipokwenda kukagua ujenzi wa nyumba hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akikagua ujenzi wa
nyumba za makazi ya wananchi katika eneo la Magomeni quotors (Kota)
katika eneo hili Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Mhe Paul MAKONDA akikagua baadhi ya vifaa vya
ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi katika eneo la Magomeni
quotors (Kota) katika eneo hili Rais Magufuli ataweka jiwe la
msingi.
Kasi ya ujenzi ni kama inavyoonekana katika picha kwa mujibu wa
mratibu wa ujenzi huu Arch Christina Shayo ujenzi wa ghorofa za chini unaelekea
kukamilika
Arch Christina Shayo akitoa maelezo jinsi Mtambo wa kuchanganyia udongo (Batching
Plant) kwaajili ya ujenzi ambao ni mpya unavyoweza kufanya kazi wakati RC
Makonda alipotembelea na kufanya ukaguzi mapema jana. Mtambo huo umefungwa na
wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao muda wowote utaanza kufanya kazi.
RC Makonda akitaka kujua jambo kuhusu mtambo wa kuchanganyia udongo (Batching
Plant).
RC Makonda akishuka kutoka juu kukagua mtambo.
RC Makonda akitoka kukagua mtambo wa kuchanganyia udongo (Batching Plant)
kwaajili ya ujenzi ambao ni mpya, Mtambo huo umefungwa na wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) ambao muda wowote utaanza kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment