Meneja wa Man Utd Jose Mourinho
amewalaumu washambuliaji wake na kuwaita ‘Wazembe’ baada ya kushindwa kuibuka
na ushindi dhidi ya Anderlecht ya Ubelgiji katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa
robo fainali wa Europa League uliochezwa kwenye uwanja wa Constant Vendon Stock
usiku wa kuamkia leo.
Man Utd
walikuwa wanaongoza muda mrefu lakini wenyeji walisawazisha dakika ya 86 na
kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya bao moja, hatua ambayo ilimkera
Mourinho.
“Kama
ningekuwa beki wa Man Utd ningekasirishwa sana na washambuliaji. Mabeki
walifanya kazi kubwa lakini waliotakiwa kumaliza mchezo walishindwa.”
“Tatizo ni
lile lile, tumecheza vizuri, tumetengeneza nafasi nyingi lakini tumeshindwa
kufunga mabao,” alisema Mourinho.
“Katika
kiingereza changu kibovu sijaona neno jingine la kuwaita washambuliaji wangu
zaidi ya ‘Wazembe’. Wanapaswa kuongeza umakini zaidi.”
“Ukiangalia
kiwango cha soka kilichoonyeshwa na wachezaji wawili ama watatu utaona haikuwa
nzuri kabisa. Marcus Rashford, Jesse Lingard, Zlatan Ibrahimovic, Anthony
Martial wote walikuwa sawa,” alimaliza Mreno huyo.
Henrikh
Mkhitaryan aliifungia Man Utd dakika ya 36 ambapo Mashetani hao walipiga
mashuti 16 langoni mwa wenyeji wao.
Man Utd
wapo nyuma kimabao dhidi ya timu zote zilizo kwenye nne bora ya ligi kuu nchini
England ambapo wamefunga mabao 46 huku timu za Chelsea, Tottenham, Liverpool,
Manchester City na Arsenal wakifunga zaidi ya mabao 60.
Zlatan
Ibrahimovic ndiye kinara wa timu hiyo baada ya kufunga mabao 28 huku wachezaji
wawili tu Mkhitaryan na Juan Mata wakiwa wamefunga zaidi ya mabao 10.
No comments:
Post a Comment