Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Maonyesho ya Jukwa la Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania jana Jijini
Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mama Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo alipotembelea banda la Kampuni ya
Supperdoll (wasambazaji wa Matairi aina ya Michellin) wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Maonyesho ya Jukwa la Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania
jana Jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi
wa Makumbusho ya Taifa. Kutoka kulia kwake ni Balozi wa Ufaransa hapa nchini
Melika Berak na Mkurugenzi Mtendaji wa Supperdoll Seif Seif (kushoto).
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bibi.
Melika Berak akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Jukwa la
Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.
Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu
Hassan.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dkt. Reginald
Mengi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Jukwa la
Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.
Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu
Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania
Bibi. Melika Berak wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maonyesho ya Jukwa la
Wafanyabiashara baina ya Ufaransa na Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.
Maonyesho hayo ya siku nne yanafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),
Dkt. Reginald Mengi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Tanzania ni Moja ya nchi
salama kwa ajili ya uwekezaji barani Afrika kwa sababu haina matatizo ya
migogoro ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa mali ya wawekezaji
ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonyesho
ya Kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia
amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Ufaransa kuja
kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa katika kilimo, nishati, utalii,usafiri
kutokana na hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.
Makamu wa Rais amesema maonyesho hayo ya
kibiashara ambayo yataambatana na kongamano kubwa la Kibiashara kati ya nchi
hizo Mbili ni fursa ya kipekee kwa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa
kukutana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya kibiashara na
uwekezaji.
Ameeleza kuwa katika kuelekea katika uchumi wa
viwanda Tanzania haiwezi kufanya kazi hiyo peke yake bali kwa kushirikiana na
mataifa makubwa ambayo yamekuwa na teknolojia ya kisasa katika uwekezaji
ikiwemo taifa la Ufaransa.
Makamu wa Rais amewahakikishia wawekezaji wote
wanaokuja kuwekeza nchini kuwa serikali itafanya kila linalowekezekana
kuendelea kujenga mazingira bora kwa ajili ya uwekezaji.
Amesema katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na
mazingira bora ya uwekezaji barani Afrika serikali imeendelea kutenga bajeti ya
kutosha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu mbalimbali ikiwemo bandari, reli,
barabara, usafiri wa anga ili kurahisisha kazi ya usafiri na usafirishaji
nchini.
Kwa upande wake, Balozi Ufaransa hapa nchini
Malika BERAK amesema kuwa ufunguzi wa Kongamano hilo kubwa la Kibiashara kati
ya Tanzania na Ufaransa linalolenga kujenga na Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara
kati ya nchi hizo Mbili.
Balozi huyo amesema kuwa kongamano hilo
litajikita katika kujadili kwa kina fursa za uwekezaji hapa nchini hasa kwenye
maeneo ya nishati, usafirishaji, teknolojia ya habari na Mawasiliano na miradi
ya maendeleo.
Kongamano hilo la siku Nne la Kibiashara kati
ya Ufaransa na Tanzania litawakutanisha wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao
wa Ufaransa katika kujadili na kubadilisha uzoefu katika masuala mbalimbali
yakiwemo ya kibiashara kama hatua ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.
No comments:
Post a Comment