Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto
James akibadilishana mkataba wa kibajeti na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU)
nchini Bw.Roeland van de Geer mara baada ya kusaini mkataba huo Jijini Dar es
Salaam.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van
de Geer akizungumza jambo na waandishi wa habari juu ya msaada wa shilingi
bilioni 486.9 uliotolewa na umoja huo kwa Serikali ya Tanzania ili kusaidia
Bajeti.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto James.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango
Bw.Dotto James akitoa ufafanuzi kwa wahandishi wa habari juu ya msaada wa shilingi
bilioni 486.9 ambao Serikali imeupata kutoka umoja wa ulaya (EU) kwa ajili ya
kusaidia Bajeti.Kushoto kwake ni Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
Bw.Roeland van de Geer.
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini
msaada wa shilingi Bilioni 490 usiokuwa na masharti yeyote kutoka Umoja wa
Ulaya ikiwa ni msaada wa kibajeti kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka wa
bajeti wa 2017/18.
Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali na Balozi wa Umoja wa Ulaya
(EU) nchini Bw.Roeland van de Geer kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kusaini mkataba huo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amesema
Umoja wa Ulaya umetoa msaada huo kutokana na kuvutiwa na juhudi za Serikali ya
Awamu ya Tano katika maeneo mbalimbali ikiwemo kupambana na rushwa na
ubadhirifu wa mali za umma.
“Nadhani mmeshuhudia utiaji saini huu ulioisha hivi
punde na Umoja wa Ulaya wametuhakikishia kuendelea kutusaidia katika masuala ya
misaada ya kibajeti pamoja na kuwa bega kwa bega na Serikali katika masuala
mbalimbali ya maendeleo”,Aliongeza Katibu Mkuu huyo.
Pamoja na hayo mpango wa pili wa maendeleo wa Taifa
wa Bajeti ya mwaka 2017/18 pia utapewa msaada na umoja huo kwani wameuona
mpango huo una tija na kuweka mkazo katika viwanda na kilimo.
Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU)
nchini Roeland Van de Geer amesema kuwa wameliangalia zaidi suala la utawala
kama eneo kuu katika mpango wa ushirikiano na Tanzania na vilevile wanatazamia
maendeleo zaidi katika maeneo ya kilimo,ujenzi wa barabara za vijijini na
nishati.
“Mkataba ambao tumeusaini utaiwezesha Wizara ya
Fedha na Mipango katika ukusanyaji wa mapato,zitaboresha uwajibikaji na
utumiaji mzuri wa mali za Serikali, na Umoja wa Ulaya unasapoti azma ya viwanda
ya Serikali ya Awamu ya Tano,”Aliongeza Roeland Van de Geer.
Amesema kuwa ushirikiano uliopo katika ya Tanzia na
Umoja wa Ulaya ni mpana sana na utaendelea kuimarika zaidi katika kipindi hiki
ambacho mageuzi ya sera yanahitajika.
No comments:
Post a Comment