Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango
Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage
wanatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na wafanyabishara Aprili 11, 2017
mjini Dodoma kwa lengo la kusikiliza changamoto zao ili zitafutiwe ufumbuzi.
Waziri wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage
Wakati akizungumza na waandishi wa habari
katika Wiki ya Kongamano la Biashara la Ufaransa na Tanzania Mwenyekiti wa
TPSF, Godfrey Simbeye amesema Rais John Magufuli amesikia malalamiko ya
wafanyabiashara na kwamba mkutano huo utasaidia kupata suluhu ya changamoto
zinazowakabili wafanyabiashara.
“Kusema kweli mazingira ya
biashara Tanzania siyo mazuri mmeona malalamiko mengi kutoka sekta binafsi,
wafanyabiashara wanalalamika kila mahali ukienda ni tatizo, kufuatia malalamiko
hayo ya siku nyingi Rais ameyasikia na kuagiza mawaziri wake kuongea na sekta
binafsi ili tutoe malalamiko yetu yote tunayoyaona katika uchumi huu unaongozwa
na utawala wake,” amesema.
Hata hivyo, Simbeye ameeleza kusikitishwa
kwake na mwitio mdogo wa Kampuni za Kitanzania katika kongamano hilo
lililokutanisha kampuni arobaini kutoka nchini Ufaransa, na kusema kuwa
zisizohudhuria zimekosa fursa nyingi za kibishara.
“Hizi kampuni
zilizojitokeza hapa ni kubwa sana zinaweza kutoa fursa kwa kampuni za Tanzania
kufanya sehemu ya shughuli wanazofanya zikafanyika Tanzania ila nilichosikitika
sijaona mwamko wa kampuni za ndani kuja kushiriki katika kongamano hili, hili
ni tatizo sababu wamekosa fursa labda hapo baadae tutawashauri waje waangalie
fursa sababu zipo nyingi sana,” amesema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Media Reginald
Mengi amewataka wafanyabiashara nchini kutokata tamaa pia kuzitumia fursa
zilizopo za kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Media Reginald Mengi
“Inatakiwa tujiamini kama
wenzetu walivyothubutu, tumechoka kusema hatuwezi sababu umasikini sio tatizo
bali ni changamoto na kwamba kila siku tuseme tunaweza,” amesema.
No comments:
Post a Comment