Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Akabidhiwa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, February 20, 2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Akabidhiwa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania, akikabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Bima Tanzania Dr. Suleiman Rashid Mohamed, baada ya kuwasilisha katika mkutano wa Wadau wa Bima Tanzania, uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 20-2-2025 na (kulia kwake) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amepokea Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima kwa Mwaka 2023 katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Verde, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika hafla hiyo, Rais Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwenye soko la bima ili kuongeza pato la taifa kupitia sekta hiyo.

Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwa wananchi kutokana na mageuzi makubwa yanayoendelea kufanyika katika sekta zote za kiuchumi.

Ili mageuzi hayo yafanikiwe, ni vema sekta ya bima iendane na kasi ya Serikali zote mbili kwa kujikita kwenye ubunifu na matumizi ya teknolojia. Watoa huduma za bima na wadau wote wanapaswa kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano.
WASANII wa Kikundi cha sanaa Chuo cha Mafunzo Zanzibar wakitowa burudani wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwasili katika viwanja vya Hotel ya Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, kwa ajili ya kupokea Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania, uliyofanyika leo 20-2-2025 katika ukumbi wa hoteli hiyo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitambulishwa Watendaji Wakuu wa Bima Tanzania na Kamishna wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt.Baghayo Saqware, alipowasili katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 20-2-2025, kwa ajili ya kukabidhiwa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania.
KAMISHNA wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware akiwasilisha Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania kwa mwaka ulioisha 31, Disemba 2024, kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 20-2-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya mkutano wa Wadau wa Bima Tanzania na kukabidhiwa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania, mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 20-2-2025.
WASHIRIKI wa Mkutano wa kupokea Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 20-2-2025.
BALOZI wa Bima Tanzania Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi. Zena Ahmed Said, akipiga makofi kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akihutubia katika mkutano wa kupokea Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania, mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 20-2-2025 na (kulia kwake) Kamishna wa Bima Tanzania Dkt.Baghayo Saqware na (kushoto kwake) Naibu Kamisha wa Bima Khadija Said.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali na kuonesha Kitabu cha Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania, baada ya kukabidhiwa, wakati wa hafla ya mkutano wa Wadau wa Bima Tanzania uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 20-2-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali na kuonesha Kitabu cha Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania, baada ya kukabidhiwa, wakati wa hafla ya mkutano wa Wadau wa Bima Tanzania uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 20-2-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalumu na Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware, baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wadau wa Bima Tanzania na kuwasilishwa kwa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Tanzania, uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 20-2-2025 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt. Saada Mkuya Salum.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages