SERIKALI ZANZIBAR YASIFU DHAMIRA YA KWELI BODI YA MIKOPO KUWAHUDUMIA WANAFUNZI KUPATA MKOPO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, February 15, 2025

SERIKALI ZANZIBAR YASIFU DHAMIRA YA KWELI BODI YA MIKOPO KUWAHUDUMIA WANAFUNZI KUPATA MKOPO

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema Bodi ya Mikopo ya Tanzania (HESLB) imeonyesha dhamira ya kweli kuwahudumia wanafunzi kwa kutoa mikopo kwa usawa bila ubaguzi wala upendeleo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Muhamed Mussa kupitia hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu Wizara hiyo, Khamis Abdalla Said alipomwakilisha katika kilele cha maadhimisho ya maonyesho ya elimu ya juu kisiwani Zanzibar.

Tumeshuhuduia maendeleo makubwa kuwahudumia wananchi, hii hii ni kutekeleza dhamira ya serikali na mikopo hii inatolewa kwa usawa bila ubaguzi,” amesema

Amesema serikalii kupitia bodi hiyo imepunguza mzigo kwa wazazi na walezi kuhakikisha watanzania wanapata eimu ya juu na utekelezaji wake umekuwa wa haki sawa bila ubaguzi.

Akizungumzia kuhusu maonyesho hayo yamekuwa na tija kwa wadau wa elimu kwani changamoto zao zimesikilizwa na kupatiwa ufumbuzi.

Amesema hatua ya sasa kuwapo maofisa wa bodi katika vyuo vya Zanzibar, kumewasaidia wanafunzi hao kutatua changamoto na kupata miongozo mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo (HESLB) Dk Bill Kiwia amesema katika safari ya bodi ya mikopo, mpaka sasa imeshatoa mikopo ya Sh8.2 trilioni kwa wanafunzi 830,000.

Amesema kuna bidhaa mbalimbali zinazotolewa na bodi hiyo ikiwamo mikopo kwa shahada na stashahada na ruzuku ya Samia Scholarship kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao.

Tunayo kila sababu katika kipindi hiki cha miaka 20, kuadhimisha na kusherehekea kwasabu ni safari ndefu tumepiga," amesema

Amesema kwa mwaka huu 2024/25 wanadhani watakaribia wanafunzi milioni moja kwasababu wanasomesha wanafunzi 247,000 na Sh787 bilioni zimetolewa kuwalipa wanafunzi hao.

Umrat Suleiman mwenyekiti wa bodi ya mikopo Zanzibar amesema zaidi ya wanafunzi 18570 wamenufaika na mkopo huo, wametoa Sh118 bilioni kuwakopesha na wamekusanya Sh24.10 bilioni.

Mmoja wa wanufaika kupitia Tasaf, Salha Bakari Said kutoka Chuo Kikuu cha Abdurahman Al Sumait ameshukuru kupatiwa mikopo wanafunzi na Tasaf kwani imekuwa link kati yao na bodi kupatiwa mikopo.

Ameomba Serikali kuendeleza mpango huo kwani sio tu watasaidia wanafunzi pekee hata jamii kwa ujumla.

Tumeambiwa kuwa mwezi wa tisa mpango huu unafika mwisho, tunaomba uendelee umesaidia wengi,” amesema.

Aisha Ali Mtumwa anayesoma kozi ya sayansi ya Elimu Sumait, ameishukuru Tasaf na bodi kwa kuwapatia mikopo huku akiomba waongezewe fedha kwa ajili ya kuwasaidia kumudu gharama zao.

Sisi nyumbani tupo wengi lakini mimi mmoja pekee ndio nimefaidika kwahiyo bado wapo wengine wanahitaji kupata msaada kama huu,” amesema Aisha

Mwanafunzi mwingine, anayenufaika na Tasaf akisoma kozi ya sanaa katika elimu, Miraji Alfan Musa amesema iwapo mpango huo ukisitishwa utaleta changamoto kubwa kwa jamii kwani mpango huo umewanufaisha wengi.

Amesema mzazi wake amepewa fedha za kujikimu na Tasaf “lakini ameanzisha biashara ya kufuga kuku, pamoja na mimi kupewa mkopo lakini kile anachokipata mzazi wangu kwenye biashara yake ananisaidia katika matumizi mengine ya kujikimu.

Amesema serikali izidi kuziangalia kaya masikini ziendelee kunufaika na iwapo mpango ukisitishwa itaumia jamii nyingi kwa silimia kubwa imekuja kuwanyanyua wenye hali ya chini, kwasasa Tanzania sio masikinia sana kwasbabu ya Tasaf.

Kwa upande Mratibu wa Tasaf Unguja, Makame Ali Haji amesema kupitia bodi ya mikopo kuanzia mwaka 2020 hadi sasa zaidi ya wanafunzi 100 kutoka kaya masikini wamefanikiwa kuingia elimu ya juu na kupata mikopo.

Amesema wanafunzi 60 wanafanya mitihani wamepatiwa mikopo kutoka bodi ya mikopo na kwa kushirikiana na bodi ya mikopo waongeze ili wapate asilimia 100 kwa wale ambao hawajapata.

Amesema katika fomu ya maombi ya mkopo bodi imeweka kipengele maalumu kumfanya mtoto atambulike ikiwa anatoka kaya masikini ambapo mwanafunzi anaingiza namba ya mpango wa kaya masikini.

Tunashukuru sana bodi ya mikopo lakini tunaomba wandelee kutengeneza wigo ili wanafunzi wengi wapate elimu na kupata mikopo ili tupate rasilimali nzuri baadaye,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages