Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Barclays Tanzania, Simon Mponji (katikati),
akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la kisasa la benki hiyo katika
jengo la Shirika la Nyumba (NHC), mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed na kulia ni Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Dk.
Suleman Mohamed.
Mkuu wa
Mauzo wa Benki ya Barclays Tanzania, (kushoto), akieleza kuhusu huduma mbali mbali za kibenki zitolewazo katika tawi jipya Barclays la mjini Morogoro
katika sherehe za uzinduzi wa tawi hilo juzi. Wengine kutoka kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji, Abdi Mohamed, mjumbe wa bodi, Dk. Suleman Mohamed na Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Barclays, Simon Mponji.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Barclays
Tanzania, Simon Mponji (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari
katika hafla ya uzinduzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo mjini Morogoro.
Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays, Abdi Mohamed na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Dk.
Suleman Mohamed.
No comments:
Post a Comment