“Siku mkiniona VEVO basi mjue nimeyakamilisha haya” – Diamond Platnumz - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, February 27, 2017

“Siku mkiniona VEVO basi mjue nimeyakamilisha haya” – Diamond Platnumz

Awali msanii wa Bongofleva Diamond platnumz hakuwepo kwenye Mtandao maarufu wa kuweka video (VEVO) na alipoulizwa alijibu kuwa uwepo wa msanii Vevo anatakiwa alipwe zaidi ya anavyolipwa kwenye upande wa Youtube.
Baada ya kujiunga Vevo Diamond February 26 ameyaandika yafuatayo >>>”Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo vevo… nikawambia uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida”
“Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hiyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo”
“Mbali tu ya kumlipa, VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo” hivyo nikawambia: “siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida.
SABABU YA KUYASEMA HAYA:
Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyezi Mungu kausaidia kuufikisha sehemu flani, hivo wasanii lazima tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu.

Vilevile umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichukua juu ya sanaa zetu kwa sasa maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae… nafahamu Wasanii wengi hawakuwa wakilifahamu hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao…”
Kwa uchungu wa kufahamu namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisameh…🙏 -SIMBA #MALENGO

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages