Wito umetolewa kwa wasanii kuacha kutumia dawa za kulevya na vileo kabla ya kuanza kufanya kazi zao,ili waweze kuongeza weledi wa sanaa kwa hadhira.
Wito huo umetolewa na mwandishi mwandamizi wa Michuzi blog Humphrey Shao, alipokuwa akizungumza na wasanii pamoja na waandishi wa habari katika jukwaa la Sanaa lililoandaliwa na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA).
Akizungumza katika jukwaa hilo ,Shao amesema kuwa amefanikiwa kuandika makala nyingi,zinazousu matatizo ya dawa za kulevya kwa wasani tangu mwaka 2014 lakini mwaka huu 2017 ndipo mambo yote yamekuwa hadharani.
“tatizo la dawa za kulevya kwa wasanii halijaanza leo, na wengi wao huanzia na kilevi cha bangi na kupelekea kujiingiza kwenye dawa za kulevya hali inayo hatarisha maisha yao na kazi zao za sanaa”amesema Shao.
Kwa upande wake msanii wa muziki wa Bongo Fleva Snura Mushi amesema kuwa, amekuwa akishuhudia wasanii wengi ambao hawawezi kupanda jukwaani mpaka walewe, hali inayopelekea wengi wao kuharibu kazi na kupoteza mashabiki.
Ametaja kuwa mtu ukitumia madawa yakulevya au pombe katika kazi yako inakufanya upoteze umakini ambao unaweza kukupoteza katika ramani ya sanaa na heshima yako kushuka.
Nae katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mwingereza ametoa onyo kwa wasanii wote ambao wanatumia dawa za kulevya na wale ambao hupendelea kunywa pombe kupita kiasi na kupanda katika majukwaa ya muziki.
Mwingereza amesema kuwa kitendo cha msanii kupanda jukwaani akiwa amelewa ni kudhalilisha kazi ya sanaa ambayo ni kazi kama ilivyo kazi nyingine na kutaja kuwa ni mara chache sana kuona wakandarasi au madaktari kuona wakiwa katika kazi zao wamelewa kama wasanii wetu.
No comments:
Post a Comment