Jeshi
ni mkusanyiko wa watu wenye fani, taaluma, uwezo na jinsia tofauti lakini wenye
lengo moja kulinda maslahi na uhuru wa nchi. Tofauti kati ya jeshi moja na
lingine ni Mafunzo, majukumu na taratibu za kazi kulingana na katika tuliyonayo
sasa.
Yale maonyesho unayoyaona uwanja wa taifa na karibuni dodoma ni
sehemu ndogo ya majeshi mbalimbali ndani yake kuna watu wa fani karibu zote
unazozijua na usizozijua. Kwa wale waliomaliza kidato cha nne au sita na kupitia au
kutokupitia JKT na kutaka kwenda Jeshi.
Tafadhali
kama umefanikiwa kufika hatua hii ya elimu, tafuta fursa ujiendeleze kwenye
fani nyingine mbalimbali kama ualimu, kilimo, uvuvi, udereva, ufundi wa vitu
mbalimbali, ushauri nasaha, ufamasia, uuguzi, usimamizi, ujasiriamali na
nyingine nyingi zilizopo.
Unapokuwa
na fani angalau moja au zaidi inaweza kuwa rahisi Zaidi kwako kujiunga na
chombo chochote kama nafasi zikitangazwa siku nyingine kama bado unania hiyo na
kama ukikidhi vigezo vya umri, afya, elimu na mengine mbalimbali. Hata pale
unapokosa basi fani unayo maisha yanaendelea na kazi mbalimbali utaendelea
kufanya.
Usijiunge
na vyombo hivi kwasababu unadhani unaweza unaweza kutoka kimaisha na ajira ni
ya uhakika – humu pia kuna risk zake nyingi pale usipofuata maadili na taratibu
zilizopo hasa pale unapokua huna nia ya dhati na uzalendo kwa nchi yako Zaidi
ya tamaa za kimaisha.
Usimpe
vyeti vyako mtu yoyote kwa kisingizio kwamba ataenda kukusaidia kukuingiza
kwenye vyombo hivi - unaweza kushangaa cheti chako kikatumiwa na mtu mwingine
kufanikisha mambo yake mengine ikiwemo kujiunga na vyuo au kupata fursa
nyingine mbalimbali – Wewe fuata taratibu zilizopo, kama fursa zimetangazwa
Omba fuata masharti na vigezo.
Angalia
mienendo yako binafsi kwenye mitandao ya kijamii vile unavyopost, changia,
share, marafiki na watu wengine wa karibu – msururu huu unaweza kuchangia
kukukwamisha kwenye mengi sio jeshi tu.
No comments:
Post a Comment