Manukato
ya mwanamuziki huyo yamepewa jina Chibu Perfume, kwa kufuata jina lake ya utani
la Chibu Dangote.
Chupa
ya manukato hayo inauzwa takribani Sh105,000 za Tanzania.
Diamond
anaonekana kuwafuata wasanii wengine mashuhuri duniani ambao wamejiingiza
katika biashara ya manukato na hutumia umaarufu wa nembo zao kujipatia mapato
zaidi.
Wakati wa
uzinduzi huo Diamond alisema kuwa ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza
manukato 'Pafyum' yenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala
zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini lakini pia kuongeza pato la
Taifa kwa kulipa Kodi.
Amesema kuwa
kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi
lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana
na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya
CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi
cha shilingi 105.000 kwa moja.
Katika
mkakati mwingine wa soko, Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako
katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways
kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa
ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege katika
nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika.
Msanii Nasseb Abdul a.k.a Diamond Platnumz
akiongozana na Mmoja wa Meneja wake almaarufu
kwa jina la Babu Tale kuelekea kwenye uzinduzi huo.
Mmoja wa Meneja wa Diamond Platnumz almaarufu kwa
jina la Babu Tale akiwakaribisha wana habari na wadau mbalimbali waliofika
kushuhudia tukio hilo adhimu la uzinduzi wa Pafyum ya msanii huyo iliyojulikana
kwa jina la CHIBU.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, ambaye amekuwa akifanya vyema
ndani na nje ya nchi (anga za Kimataifa), Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz
akizungumza mbele ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine waliohudhuria
hafla fupi iliyohusu uzinduzi wa manukato (Pafyum) yake iliyoitwa CHIBU, mapema
jana jijini Dar.
Msanii Nasseb Abdul a.k.a Diamond Platnumz
akimkabidhi chupa ya Pafyum, mteja wake wa kwanza aliyejitambulisha kwa jina la
Aisha Azori, wakati wa uzinduzi huo.Mwana mama huyo alionekana kujisikia fahari
kununua bidhaa ambayo imetengenezwa na Msanii wa hapa nyumbani,ambae pia
anafanya vyema katika kazi zake za Muziki.
Msanii Diamond akisikiliza jambo kutoka kwa mwandishi wa habari, kushoto ni Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz
almaarufu kwa jina la Babu Tale.
Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz almaarufu kwa
jina la Babu Tale akiongea jambo kwa waandishi wa habari.
Meneja wa Diamond Plutnamz Bw. Salaam Medes akizungumza mara baada
ya kuzindua pafyum hiyo kwenye duka kubwa la GSM Mall barabara ya Nyerere
jijini Dar es salaam leo.
Msanii
Diamond akifafanua jambo kwa Wanahabari
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha Pafyum ya
CHIBU ambayo ndiyo kwanza imeingia sokoni.
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha Pafyum ya
CHIBU ambayo ndiyo kwanza imeingia sokoni.
Bw. Salaam Mendes akitaja bei ya pafyum hiyo kwa waandishi wa
habari mara baada ya kuizindua rasmi jana jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Diamond alipokuwa
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Pafyum hiyo ambayo tayari imekwisha sambaza
kwenye maduka mengi jijini Dar.
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha Pafyum ya
CHIBU ambayo ndiyo kwanza imeingia sokoni na kusisitiza jambo juu ya sifa za Pafyum hiyo.
Mwanamuziki Baseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akizungumza na
waandishi wa habari wakati akizindua Pafyum hiyo kulia ni Mmoja wa Mameneja
wake Babu Tale.
No comments:
Post a Comment