Rouhani alishinda kwa kura nyingi sana
uchaguzi wa mwaka 2013
Rais wa zamani Mahmoud
Ahmadinejad hata hivyo amezuiwa kuwania na jopo hilo linalowachuja wagombea
ambalo linadhibitiwa na serikali.
Mshirika wa karibu wa
Ahmadinejad Hamid Baghaie pia amezuiwa kugombea urais.
Orodha kamili ya wagombea
kwenye uchaguzi huo wa tarehe 19 Mei itatangazwa 27 Aprili.
Wagombea zaidi ya 1,600
walitaka kuwania lakini ni sita pekee ambao walichaguliwa na Baraza Kuu la
Walinzi.
Kuidhinishwa kwa Bw Rouhani na
Bw Raisi kunatarajiwa kusababisha mvutano mkali wa kisiasa kati ya kambi zao
mbili.
Bw Rouhani alichaguliwa kwa
kura nyingi mwaka 2013, ambapo aliahidi kufikisha kikomo kutengwa kwa taifa
hilo kidiplomasia katika jamii ya kimataifa na kuhakikisha uhuru zaidi wa
kijamii.
Miaka miwili baadaye, serikali
yake na nchi nyingine sita za Magahribi zilifikia mkataba wa kihistoria kuhusu
mpango wa nyuklia wa Iran, ambapo Iran ilikubali kusitisha mpango wake wa
kustawisha silaha za nyuklia na mataifa ya Magharibi nayo yakaondoa vikwazo.
Bw Raisi ni seyed, mtu ambaye
anaweza kufuata historia ya ukoo wake hadi kwa Mtume Muhammad.
Ana sifa za kuwa na msimamo
mkali kuhusu masuala mengi muhimu na inadaiwa anaungwa mkono na Kiongozi Mkuu
wa Kidini Ayatollah Ali Khamenei.
Ahmadinejad, ni mtu pia mwenye
msimamo mkali ambaye alihudumu kwa mihula miwili kama rais kati ya 2005 na
2013.
Alishangaza wengi alipojiandikisha
kuwa mgombea wiki iliyopita licha ya kushauriwa na Khamenei asiwanie.
Wengine wanaowania ni Mostafa
Mirsalim, meya wa Tehran Mohammad Bagher Ghalibaf, Mostafa Hashemitaba na
Makamu wa Rais Eshaq Jahangiri.
No comments:
Post a Comment