Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe
akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka la Airtel mkoa wa Manyara.
wakishuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa Airtel.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe
akiongea mara baada ya kuzindua duka la Airtel Mkoani Manyara akishuhudia
Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara Peter Kimaro.
Afisa wa kitengo cha huduma kwa wateja wa dula la
Airtel Manyara Bi Ramla Rajabu akimuonyesha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,
Francis Massawe baadhi ya simu zinazopatikana katika duka jipya lililopo Babati
mjini mara baada ya kuzinduliwa kwa duka hilo jipya litakalotoa huduma kwa
wateja na wakazi wa mkoa wa Manyara.
Kampuni ya simu za
mikononi ya Airtel imezindua duka mjini Babati kwa ajili ya kutoa huduma kwa
wateja wanaoishi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Manyara ikiwa ni
mwendelezo wa mpango wake wa kufungua maduka ya kutoa huduma kwa wateja wake
nchi nzima.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Manyara,Fransic Masawe,ndiye aliyezindua duka hilo ambaye amesema litasadiai
kutoa huduma kwa wakati lakini pia lisaidia kutoa ajira kwa vijana na
kuwawezesha wakulima wa mazao ya kupata huduma za kifedha kwa urahisi
zaidi.
“ nawapongeza
Airtel kwa kusogeza huduma karibu na wateja na kuongeza kuwa duka hilo
litakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mji wa Babati pamoja na maeneo
jirani. Napenda kuchukua fursa hii kuwa kuwaasa wakazi wa hapa hususani vijana
kuchangamkia fursa za ajira zilizopo kupitia duka hilo ajira kwa lengo
lakujiongezea kipato”. Alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Fransic
Masawe.
Kwa Upande wake
Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara,Peter Kimaro,amesema duka hilo linalenga
kusogeza huduma karibu na jamii kwani kipindi cha nyuma wananchi walikuwa
wanapata tabu kupata huduma za uhakika lakini pia hatua hiyo inatoa mwanya
wakuongeza maduka mengine mengi katika maeneo ya mkoa huo ikiwemo wilaya
ya Katesh.
Pia amesema huduma ya
mawasiliano ni chachu ya maendeleo kwani inasaidia uendeshaji wa shughuli za
kiuchumi na kuwawezesha huduma za kifedha kupatikana kirahisi ambapo kwa sasa
watu wengi hutumia Airtel Money kufanya miamala pamoja na kupata mikopo kupitia
huduma ya Airtel Timiza ambayo imekuwa ni mkombozi kwa wajasiriamali wadogo
wadogo kupata mitaji ya kuendesha biashara zao.
Tunatoa wito kwa wateja
wetu kutembelea maduka haya ambayo tunayafungua nchi nzima ili kupata huduma
hapa manyara tayari tunayo maduka matatu ambayo moja tunalizindua hapa na
mengine mawili yapo katika maeno ya Dareda center na Riloda aliongeza Kimaro.
Baadhi ya wananchi
wamesema kufunguliwa kwa duka hilo kutaongeza ajira kwa vijana pamoja na kutoa
huduma za uhakika za miamala ya fedha na mawasiliano kwa ujumla tofauti na
kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wanalazimika kufuata huduma umbali mrefu
kidogo.
Kampuni ya Airtel
inampango wakuongeza maduka mengine katika mkoa huo wa Manyara ili kuendelea
kusogeza huduma zake kwa wateja kwa urahisi hususani katika maeneo ya vijijini.
No comments:
Post a Comment