Bw Motlanthe ameiambia BBC
kuwa, kura yake kwa ANC haifai kuchukuliwa kama 'iliyotiwa kwenye kapu' itapotimia
uchaguzi mwaka wa 2019.
Bw Motlanthe, ambaye alihudumu
kwa muda mfupi kama rais kati ya 2008 na 2009 na alikuwa wakati mmoja wa naibu
wa rais Zuma, aliashiria kuwa alijaribu kumshawishi kiongozi huyo kuondoka
mamlakani zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Aliongeza kuwa hafurahishwi na
mtazamo wa baadhi ya mawaziri wa kutojali masuala ya uchumi wa nchi, huku
waziri mpya wa fedha akijaribu kutuliza hofu katika mkutano wa Benki ya dunia
mjini Washington (Ijumaa) kufuatia kushuka kwa kiwango cha uchumi nchini Afrika
Kusini.
Ijapokuwa Kgalema Motlanthe
alikuwa kidogo asaliti chama chake ambacho amehudumu kwa miaka mingi, alisema
kura yake kwa ANC "haingepeanwa" wakati wa uchaguzi mkuu mwaka wa
2019.
Bwana Motlanthe ni mmojawapo wa
viongozi wa kwanza watajika kushuku hali ya baadaye ya ANC chini ya uongozi wa
Jacob Zuma ambaye alikuwa rafiki wake wa karibu katika uongozi.
Zuma atakumbana na kura ya
kutokuwa na imani Bungeni mwezi ujao huku upinzani ukionekana kuwa mkali -
ijapokuwa bado ana ushawishi mkubwa maeneo ya mashambani.
Atakayemrithi Zuma kama
kiongozi wa ANC atachaguliwa na chama mwishoni wa mwaka lakini Kgalema
Motlanthe amedokeza kuna haja ya dharura.
Alisema ANC " inazama kwa
makosa iliyofanya ambayo yamefurika" na kutabiri kuwa kumuunga mkono
kiongozi wake itamaanisha kwa uhakika kwamba ANC itapoteza utawala wa wengi
katika uchaguzi miaka mbili zijazo.
No comments:
Post a Comment