Naibu Waziri wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla,
amewatunuku vyeti wanafunzi wa kike 25 wa shule mbalimbali za sekondari
waliofanya vizuri katika mafunzo ya uchambuzi wa takwimu.
Dk. Kigwangallah ametoa
vyeti hivyo leo kwa wanafunzi hao baada ya mafunzo ya siku tatu ya namna ya
kutumia takwimu.
Mafunzo hayo yameandaliwa
na kufadhiliwa na DataLab-dlab kwa kushirikiana na UDICTII, Apps Girls and She
Code for change na yamelenga kuwajengea uwezo kwenye eneo la kutumia takwimu,
kuzitafsiri na kuziweka kwenye taarifa ambazo zinaweza kutumika na walaji kama
vile wanahabari, wabunge, watunga sera na wengine wenye uhitaji.
Dk. Kigwangallah
amewapongeza waandaji na kueleza kuwa yatawajenga watoto kwenye utamaduni wa
kutumia takwimu.
Mkuu wa Mafunzo wa Mradi
wa Takwimu, Tanzania, Mahadia Tunga, ambaye ni Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu
cha Dar es salaam, amesema wameamua kutoa mafunzo hayo ya uchambuzi wa takwimu
kwa watoto wa kike sababu mara nyingi mwamko wao huwa ni mdogo tofauti na
wanaume.
Amesema kuwa mafunzo hayo
wanayatoa kwa watoto kuanzia umri wa miaka 15 hadi 20 ili kuwajengea uwezo wa
kukabiliana na changamoto na kuzipatia ufumbuzi.
Caroline Ndosi akizungumza na
Washiriki.
Wasichana Walioshiriki katika
Mafunzo wakifatilia hotuba ya Naibu waziri
Mhitimu kutoka Shule ya
Sekondari Jangwani, Sheila Juma akizungumza na juu ya programu yake amabyo
ameigundua mara baada y kufanya mafunzo kutoka Tanzania data Lab.
Mmoja wa Washiriki katika
mafunzo hayo, Necta Richard akizungumza juu ya progamua mabyo ameizindua mara
baada y kupata mafunzo.
Mkuu wa Mafunzo kutoka Tanzania
Data Lab , Mahadia Tunga akizungumza na Washiriki waliopata mafunzo hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya
pamoja na washiriki wa mafunzo ya tehema kutoka Tanzania Data Lab.
No comments:
Post a Comment