Baada ya kukaa kimya kwa
miezi mingi bila kuachia wimbo, Hussein Machozi anatarajia kuachia wimbo mpya
wiki chache zijazo. Wimbo huo unajulikana kwa jina la ‘Nipe Sikuachi.’
Wimbo huo umetayarishwa
na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa Bongo Flava katika miaka tofauti,
Man Walter kupitia studio zake za Combination Sound.
“Combination ya mimi na
Man Walter, sidhani kama kuna kitu cha mchezo hapo,” anasema Machozi ambaye amethibitisha
kuanza kufanya kazi rasmi kwa uangalizi wa label ya mtayarishaji huyo mashuhuri
nchini Tanzania.
“Man Walter ni mshkaji
kitambo, tumekutana tukakubaliana kufanya kazi na tukaona kabisa kwamba sisi
tukifanya kazi wawili itakuwa kazi na ndicho kilichofanyika japo tuna
makubaliano ya kusaini. Kwahiyo ni mimi tu nirudi Tanzania tuje tukae tusaini,
lakini ukweli ni kwamba mimi nafanya kazi chini ya uongozi wa Kombinega,” amesema.
“Video pia imefanyika
Italy, Gressoney Italy.Kuna mabadiliko makubwa ukiangalia location ambazo
tumezizoea, ukiangalia video ambazo kila siku tunaziona Tanzania za magari na
majumba,” amesisitiza muimbaji
huyo.
Machozi ambaye
anafahamika kwa vibao vingi vilivyowahi kufanya vizuri kwenye vituo vya redio
na runinga ndani na nje ya Tanzania vikiwemo ‘Utaipenda’, ‘Kwaajili Yako’, ‘Addicted’ na zingine, amedai kuwa
ukimya wake ulitokana na majukumu mengine ya kimaisha.
“Kama unavyojua, hakuna
mtu anapenda kuwa kimya, na ukifuatilia vizuri kuna kazi kadhaa nilishawahi
kuziachia lakini hazikufika nilikotarajia nadhani kwasababu ya ukosefu wa
management.
Kwa sasa Hussein anaishi
nchini Italia baada ya kuwa ameenda kusoma, lakini hiyo haimaanishi kuwa ameupa
kisogo muziki, kitu anachoamini alizaliwa kukifanya.
“Ilikuwa ni kozi fupi
ambayo kwa sasa imeisha na nafanya shughuli za kawaida kujipatia riziki,” anaeleza.
Machozi anakikisha kuwa
ujio wake mpya utakuwa wa tofauti.
“Kinachokuja kuonekana
sasa hivi, hakijawahi kuonekana katika macho ya watu na nimejaribu kufanya
hivyo kwasababu mimi mwenyewe nahitaji mabadiliko, nifanye kitu ambacho ni
kipya zaidi hata kwenye macho yangu mimi, kwahiyo nimekikubali kwamba ni kipya,
video ni mpya, audio ni mpya kabisa.”
Anasema tarehe rasmi ya
kutoka kwa video na wimbo itatangazwa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment