Siku
ya tarehe 21 ya mwezi April mwaka 1926 ndipo Malikia Elizabeth wa II alizaliwa.
Jina
halisi la Malkia ni Elizabeth Alexander Mary Windsor.
Malikia
Elizabeth alitambuliwa kama Malkia baada ya kifo cha baba yake mzazi ambapo kwa
wakati huo yeye alikua nchini KENYA katika ziara ya kutembelea mbuga za wanyama
na pia kukutana na Machifu wa huko.
Akiwa
nchini Kenya alianza kupewa ulinzi maalum kama Malkia mara baada ya taarifa za
kifo cha baba yake mzazi na itifaki zote za kiutawala zilianza kutekelezwa
akiwa nchini Kenya.
Amekuwa
Malkia wa UK tokea mwaka 1952. Akiwa na umri wa miaka 25 tuu hadi sasa ambapo
ameshatimiza jumla ya takriban miaka 91 tokea kuzaliwa kwake. Ni Kiongozi pekee
katika familia ya kifalme UK kutawala kwa muda mrefu.
Malikia
mbali na UK pia ni kiongozi wa nchi nyengine huru 12 ambazo ni Jamaica,
Barbados, the Bahamas, Grenade, Papua New Guinea, Solomon Islan, Tuvalu, Saint
Lucia, Saint Vicente and the Grenadines, Belize, Antigua and Barbuda na Saint
Kitts and Nevis.
Malkia
Elizabeth pia ni Mkuu wa jumuia ya Madola yenye nchi 52 zikiwemo Tanzania,
Kenya, Uganda, Zambia, Malawi na nyenginezo.
Malkia
Elizabeth, Anahudumia zaidi ya taasisi 600 za kujitolea na mashirika ya hiari.
Mamlaka
na nguvu za Malikia Elizabeth:
1. Bila
ya ruhusa yake hakuna mswada wa sheria unaweza kupitishwa kuwa sheria.
2. Alituma
ujumbe wa pongezi kwa wana anga wa APOLO II walipokanyaga mwezini, ujumbe huo
umehifadhiwa katika kifaa maalum cha chuma huko huko.
3. Anaweza
kusafiri bila hati ya kusafiria nje ya nchi yake.
4. Anaweza
kuendesha gari bila leseni wala nambari za gari.
5. Ana
mtunga mashairi wake makhsusi.
6. Ana
ATM machine ya kutolea pesa ya kwake binafsi.
7. Anauwezo
wa kutolipa kodi.
8. Anauwezo
wa kumuonya waziri yeyote na hata kumuwajibisha.
9. Ni
Mwenyekiti wa Kanisa la Anglikana.
10. Ana
uwezo wa kuvunja serikali ya Australia.
11. Ana
kinga ya kushitakiwa.
12. Anamiliki
ndege aina ya swans.
13. Ana
uwezo wa kumteua Spika kwa amri yake.
14. Malkia
Elizabeth, katika historia ndie Kiongozi wa nchi aliewahi kusafiri zaidi nje ya
nchi yake duniani kwote.
15. Meli
za jeshi la wanamaji za Uengereza huitwa kwa majina yanayotokana na Malkia, kwa
mfano HMS (Her Majesty Ship).
Malkia
Elizabeth ndie mtu pekee duniani anaesherehekea siku yake ya kuzaliwa mara
mbili kwa mwaka yaani tarehe kama ya leo 21, Aprili na jumamosi ya julai.
Kila la kheri kwako Malkia Elizabeth
II (Malkia Elizabeth Alexandra Mary Windsor)
No comments:
Post a Comment