Meneja Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi, akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini, uliofanyika hii leo Buzuruga Plaza Jijini Mwanza.
Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania,
Judie Wu, akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King
nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii mapema jana.
Mgeni Rasmi, Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana
mkoani Mwanza, Zubeda Kimaro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
John Mongella, kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini
Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro
(mwenye kofia), akizindua ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi
rasmi wa kampuni hiyo kimataifa hii leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa
kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu.
Baadhi ya maafisa wa taasisi hiyo na wageni waalikwa wakifuatilia
uzinduzi huo.
Wakazi wa maeneo ambayo
bado hayajafikiwa na huduma ya umeme nchini, wanatarajiwa kunufaika na huduma
hiyo kupitia mitambo ya umeme wa jua kwa bei nafuu inayosambazwa na kampuni ya
Sun King.
Meneja Masoko wa kampuni
hiyo nchini, Albert Msengezi, ameyabainisha hayo hii leo Jijini Mwanza kwenye
uzinduzi rasmi kitaifa wa bidhaa za Sun King ambazo ni taa za sola pamoja na
majiko bunifu ya Jikokoa.
“Kila Kijiji nchini
tunakusudia kuwa na mawakala wa kampuni ya Sun King ambao watawafikia wananchi
wote wanaoishi katika maeneo hayo na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu
tunakusudia kuwa na wanufaika zaidi ya Milioni Moja ambapo tumejikita kwenye
bidhaa bora zisizochafua mazingira ikiwemo taa za sola na majiko yasiyochafua
mazingira”. Amebainisha Msengezi.
Mkuu wa Masoko wa kampuni
ya Sun King, Judie Wu, amesema kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha kila mmoja
Mjini na Vijijini anapata huduma ya umeme pamoja na kutumia majiko bunifu
yasiyo na madhara kiafiya kwa bei nafuu.
Akizungumza kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye uzinduzi huo wa bidhaa za King Sung, Zubeda
Kimaro ambaye ni Afisa Tawala wilayani Nyamagana, amewahimiza wawekezaji
kujitokeza kwa wingi kuwekeza mkoani Mwanza kwani kuna fursa nyingi za
kiuwekezaji hatua ambayo pia itazalisha ajira zaidi kwa vijana wetu.
No comments:
Post a Comment