Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imezindua jukwaa
la uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa wanawake wa Wilaya ya Handeni kwenye
ukumbi wa maount Ilulu uliopo Kabuku mjini lenye ujumbe wa “Wezesha
wanawake kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda”.
Jukwaa hili linalengo la kuwakutanisha wanawake
pamoja na kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika
biashara na shughuli nyingine za kiuchumi katika Wilaya ya Handeni.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Jukwaa hilo
Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni Bw. John
Mahali aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin
Gondwe alisema kuwa jukwaa la wanawake hilo litasaidia kuongeza
uelewa kwa wanawake katika upatikanaji wa mitaji ,
sheria za nchi katika masuala ya kiuchumi na jinsi ya kujitegemea.
Aliongeza kuwa wanawake wamekuwa hawapati fursa za
kutosha za kiuchumi hapa Nchini hata na duniani kote kutokana na kutokuwa na
usawa katika fursa , uwezo wa kupata mitaji.
“jukwaaa litasaidia kuondoa matabaka na sheri
ambazo zitasaidia kupunguza ubaguzi wa kiuchumi kwa wanawake, ambalo ni jambo
la muhimu sana katika kuleta maendeleo ya usawa katika pato la Taifa, jamii na
familia” alisema Bw. John.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe alisema kuwa jukwaa
hili litafanya kazi ya kutambua shughuli za kijasiliamari katika kutoa elimu
kuhusu upatikanaji wa mitaji, kusajili biashara, kuwezesha kiuchumi na kutafuta
masoko.
Aidha, alisema katika suala la utoaji mikopo
vikundi vitakavyopewa kipaumbele ni vile viliyojidhatiti kwa kusajiliwa, vyenye
utawala unaoeleweka, miradi inayoonekana na zenye hesabu za kifedha zinazoweza
kukaguliwa na kukosolewa inapobidi.
Uzinduzi huo ulipambwa na maonesho ya bidhaa za
kijasiliamari ya vikundi mbalimbali kutoka kata mbalimbali. Sekretarieti ya
Mkoa wa Tanga itaratibu shughuli zote za uchumi kwenye Wilaya zote ndani ya
Mkoa na kuhakikisha kunakuwa na majukwaa ya Wilaya/Halmashauri zote ambayo
yatafanya vikao vyake kila baada ya miezi sita (6).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw William Makufwe wakwanza kulia
akifuatiwa na Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali wakitazama Moja ya bidhaa ya
vikapu vinavyotengenezwa na kikundi cha wanawake tupendane cha segera.
Katibu tawala
Wilaya Bw John Mahali akizungumza na wanawake waiojitokeza kwenye Uzinduzi wa
jukwaa Hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji Bw William Makufwe akionesha katiba waliyopewa viongozi wa jukwaa la
kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya itakayowasaidia Katika Uongozi wao.
Mwenyekiti
wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya Bi Fatuma Zuberi akipokea
katiba kutoka Kwa mgeni rasmi Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali.
Mwenyekiti
wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya Bi Fatuma Zuberi akishukuru
wanawake waliompa dhamana ya kuwaongoza.
Baadhi ya
vikundi vya wanawake waliojitokeza kuonesha bidhaa zao wakati wa Uzinduzi.
Baadhi
ya wanawake wakishiriki wa Uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi
Wilaya ya Handeni.
Viongozi
wakipata maelezo kutoka vikundi vya kinamama.
No comments:
Post a Comment