Sehemu ya Makaburi ya
Mashujaa wa Tanzania, waliokuwa mstari wa mbele kuitetea Tanzania, kuhakikisha
wanamuondoa Nduli Idd Amini, hapa wakiwa wamelazwa.
MWISHO
WA VITA VYA KAGERA
Jumatano
ya Aprili 11, 1979,
Rais wa Uganda Idi Amin
Dada Oumee aliikimbia nchi yake na kwenda Libya na baadaye Saudi Arabia, baada ya kushindwa vita dhidi ya Tanzania.
KISA
CHA VITA
Uhusiano wa Tanzania na
Uganda ulidorora tangu Januari 25, 1971, Idd Amin Dada(tamka Dadaa)
alipoipundua serikali halali ya Rais Milton Obote aliyekuwa nchini Singapore
kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola.
Rais wa Tanzania, Julius
Nyerere, akampa Obote na wenzake 2000 hifadhi ya kisiasa. Idd Amin
hakufurahishwa na hilo kwani aliamini kwamba Nyerere anamuandaa Obote aje
kumpindua, kwa hiyo akapanga kumdhibiti kabla hajampindua...akaivamia Tanzania.
MIKAKATI
Kanali, Abdu Kisuule,
aliyekuwa mshirika wa karibu wa Idd Amin na kiongozi wa moja ya vikosi vya
Uganda kwenye vita hiyo, aliongea na mtandao wa www.thecitizen.co.tz kwenye
mfululizo wa makala za 'hadithi ambayo haikuwahi kusimuliwa ya vita vya Kagera'
(The untold story of Kagera War by TZ Uganda top soldiers).
"Nilitumwa Ulaya
kununua silaha, nilikuwa na wenzangu, Yekoko na meja Ndibowa. Tulikwenda Bilbao
Hispania. Tulitumwa kununua vifaru, bomu aina ya Napalm ambalo ni maalumu kwa
ajili ya kupambana na saba saba ya Tanzania(mtambo wa kurushia maroketi
uliotengenezwa Urusi uliokuwa ukiitwa BM Katyusha rocket launcher), na ndege
112 za kuangushia mabomu.
Kwa bahati mbaya, kila
tulipoenda, Tanzania ilitufuatilia na kuzima jaribio letu la kununua(Tanzania were
tracking us and blocking our orders). Endapo tungefanikiwa kununua bomu la
Napalm, habari ingekuwa habari nyingine kwa sababu Napalm ni bomu la moto
ambalo huunguza kila kitu, linapotua. Wakati bado tukiwa Hispania, Tanzania
ikavamia Uganda"
VITA
YENYEWE
Januari 30, 1978, majeshi
ya Idd Amin yalivamia Tanzania na kuvunja daraja la mto Kagera linalouunganisha
mkoa wa Kagera na sehemu nyingine ya Tanzania. Amin akautangaza mkoa wa Kagera
kama sehemu ya Uganda.
Rais wa Tanzania, Julius
Nyerere akamsihi Amin kuondoa majeshi yake...Amin akakataa. Nyerere akaziomba
jumuia za kimataifa kulaani uvamizi wa Idd Amin lakini dunia ikakaa kimya.
Nyerere akatangaza vita
vilivyoanza Oktoba 30, 1978.
UWANJA
WA MAPAMBANO
Nyerere alikusanya jeshi
la wananchi lililoanza na askari pungufu ya 40,000 na kuongezeka mpaka 100,000
wakiwemo polisi, askari magereza, JKT na migambo
Jeshi hilo likaungana na
vikundi mbalimbali vya waganda vilivyokuwa vikimpinga Amin ambavyo vilikutana
mjini Moshi kwenye mkutano wao waliouita Moshi.
Mkutano huo ndiyo
ulioanzisha jeshi lililoitwa Uganda National Liberation Army (UNLA).
Makundi haya ni pamoja na
Kikosi Maalum kilichokuwa chini ya Tito
Okello (huyu ndiye aliyeongoza Mapinduzi ya Zanzibar 1964) na David Oyite Ojok.
Pia kulikuwa na kikundi cha FRONASA kilichokuwa chini ya Yoweri Museveni,
pamoja kikundi kingine kama Save Uganda Movement.
Majeshi ya Tanzania
yalikuwa na mzinga kutoka Urusi ulioitwa BM Katyusha rocket launcher (nchini ulikuwa
ukifahamika kama saba saba) ambao ulivurumishwa moja kwa moja kwa majeshi
Uganda. Majeshi ya Uganda yarudi nyuma.
MUAMMAR GADDAFI NA
PALESTINA WAMSAIDIA IDD AMIN
Kiongozi wa Libya Muammar
Gaddafi, alituma wanajeshi 2,500 kumsaidia Idd Amin. Wanajeshi hao walikuwa na
silaha za kisasa kama vifaru vya T-54 na T-55, BTR APC, BM-21 Grad MRL,
artillery, MiG-21, pamoja na kombora la Tu-22.
Hata hivyo, walibya hao
na wapalestina wakajikuta peke yao mstari wa mbele huku wanajeshi wa Uganda
wakirudi nyuma. Askari wa Libya pamoja na Palestina wakatekwa.
Hayati
Muammar Gaddafi akisalimina na wanajeshi wa jeshi la Idd Amin wakati wa vita ya
Kagera. Idd Amin (katikati) akiwa anashuhudia.
MWISHO WA
VITA
Vita hiyo
ilianza Oktoba 30, 1978 na kumalizika Aprili 11, 1979.
Baada ya vita hii,
Gaddafi akamuomba Nyerere awaachie askari wake na yeye atampa pesa nyingi au
mafuta. Nyerere akakataa akisema binadamu halinganishwi na chochote, akawaachia
bure askari wale ambao walisifu sana jinsi walivyotendewa wakati walipokuwa
mateka.
Baadhi
ya mabaki na kumbukumbu ya magari na mabomu yaliyotumika katika Vita ya Idd
Amin mwaka 1978 - 79.
No comments:
Post a Comment