Hiyo
ndiyo mihadhara ya mwanzo kutetea sayansi, iliyoanza New Zealand na Australia,
ambako maelfu walishiriki kupinga kile wanachoona kuwa mashambulio yanayozidi
ya wanasiasa, kupinga ukweli na ushahidi.
Baadhi
yao walivaa makoti meupe ya maabara, na kubeba mabiramu kusema, "tunataka
watu wanaotafakari siyo wanaokanusha'.
Waliopanga
shughuli hiyo kimataifa, wanasema kilichowachochea kuchukua hatua, ni mipango
ya Rais Trump kupunguza sana bajeti za idara za sayansi za Marekani.
Wanasema
sayansi ni msingi wa maisha ya kawaida, haifai kuidhoofisha.
No comments:
Post a Comment