Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba
akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo-IFAD
wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bw. Sana Jatta alipofika Wizarani
tarehe 28 Aprili, 2017. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya
kuendeleza miradi ya kilimo na ufugaji hapa nchini kwa ajili ya kujihakikishia
usalama wa chakula na lishe bora kwa maendeleo.
Sehemu ya ujumbe
kutoka Ofisi za IFAD hapa nchini alioambatana nao Bw. Jatta. Kulia ni Bw.
Francisco Pichon, Mwakilishi na Mkurugenzi wa IFAD nchini akiwa na Bi. Mwatima
Juma Afisa Miradi Mwandamizi wa IFAD nchini.
Bw. Jatta nae
akimweleza jambo Mhe. Dkt. Susan wakati wa mazungumzo yao.
Sehemu ya ujumbe
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka
kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Jestas
Nyamanga, Bi. Eva Ng'itu, Afisa Mambo ya Nje na Bw. Charles Faini, Msaidizi wa
Naibu Waziri.
Mhe. Dkt. Kolimba
katika picha ya pamoja na wageni wake.
No comments:
Post a Comment