Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa
Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama
Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa
Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na
baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa
Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiweka jiwe la msingi
Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi
mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina
ya baadhi ya wataalamu mbalimbali waliohusika katika mchakato wa Ujenzi huo wa
Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani
Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza. Wakwanza kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja
Kadogosa akiwa ameshika majina hayo.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akichota mchanga na kuweka kama ishara ya
kushiriki katika ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia
jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na
Mwanza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kibao
cha jiwe la msingi cha Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia
jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na
Mwanza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa
Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Mama Janeth Magufuli
wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati
akielezea kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini
Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amechuchumaa
kwenye mfano wa Reli ya Kisasa (SGR) na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja
Kadogosa, Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Miundombinu Profesa Norman Sigala mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa Reli hiyo, wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli pamoja na Hawa Ghasia (Mb).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa
Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati akipita katikati ya
mfano wa Reli hiyo itakayojengwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono
wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya
Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na
baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Mfano
wa Reli hiyo ya Kisasa ya Standard Gauge SGR itakayojengwa kuanzia Dar es
Salaam hadi Morogoro na baadae kuendelea hadi mikoa ya Mwanza na Kigoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Kaimu Mtendaji Mkuu wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati akielekea kuweka jiwe la
Msingi ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya
kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na
Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakary Zubeiry mara baada ya kuweka jiwe la
Msingi katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza msanii Mrisho Mpoto
mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Pugu
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha
mahudhuria ya kushiriki uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia
jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya
Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 12 Aprili, 2017 ameweka
jiwe la msingi la ujenzi wa sehemu ya kwanza ya reli ya kati kwa kiwango cha
kisasa (Standard Gauge) itakayoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro, yenye urefu
wa kilometa 300 zinazojumuisha vituo vya kupishana treni na vituo vya abiria na
mizigo.
Sherehe za uwekaji jiwe la
msingi zimefanyika Pugu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali wakiwemo, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa, Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigalla King, Mabalozi wa nchi mbalimbali,
wawakilishi wa taasisi za kimataifa na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Reli inayojengwa itakuwa na
uwezo wa kubeba mizigo yenye uzito wa tani 35 kwa ekseli moja, itasafirisha
abiria kwa mwendokasi wa hadi kilometa 160 kwa saa, mizigo kwa mwendokasi wa
hadi kilometa 120 kwa saa na itakuwa na uwezo wa kusafirisha jumla ya tani
milioni 17 za mizigo kwa mwaka, ikilinganishwa na reli nyembamba iliyopo sasa
iliyojengwa mwaka 1912 ambayo inasafirisha abiria kwa mwendokasi wa kilometa
chini ya 30 kwa saa, inabeba tani 13 kwa ekseli moja na ina uwezo wa kubeba
jumla ya tani milioni 5 tu za mizigo kwa mwaka.
Sehemu ya kwanza ya ujenzi
wa reli hiyo inayofanywa na kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki kwa kushirikiana
na Motaengil Africa imepangwa kuchukua muda wa miezi 30 kuanzia sasa kwa
gharama ya Shilingi Trilioni 2.7 na itafuatiwa na sehemu nyinyine nne
zitakazounganisha reli kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa urefu wa jumla ya
kilometa 1,219.
Akitoa taarifa kwa Mhe.
Rais, Mtendaji Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini (RAHCO) Bw.
Masanja Kadogosa amesema reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba treni inayovuta
mabehewa 100 ya mizigo yenye urefu wa kilometa 2 kwa mpigo na kwamba mizigo
itakayobebwa na treni moja ni sawa na mizigo ambayo ingebebwa na malori 500.
Ameongeza kuwa kupitia reli
hiyo abiria wataweza kusafiri kati ya Dar es Salaam na Morogoro kwa muda wa saa
2 na dakika 50.
Mhe. Rais Magufuli amesema
Watanzania wana kila sababu ya kujivunia kuanza kwa ujenzi wa reli hiyo kwa
kuwa itasaidia kurahisisha usafiri wa abiria na mizigo ndani ya nchi na kwenda
nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
itazalisha ajira za moja kwa moja kwa Watanzania 600,000 na itasadia kuimarisha
uchumi.
Mhe. Dkt. Magufuli amesema
pamoja na kuanza kwa ujenzi wa kilometa 300 za kuanzia Dar es Salaam hadi
Morogoro, Serikali imeelekeza jitihada zake kuanza ujenzi wa sehemu ya pili ya
kuanzia Morogoro hadi Dodoma yenye urefu wa kilometa 336 na kwamba Serikali ya
Uturuki imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga sehemu hiyo.
Kwa wakazi wa Dar es
Salaam, Mhe. Rais Magufuli amesema katika kipindi kifupi Serikali ya Awamu ya
Tano imechukua hatua madhubuti za kuboresha Jiji kama alivyoahidi zikiwemo
kujenga barabara za juu katika makutano ya barabara maeneo ya TAZARA na Ubungo
(Flyover), kujenga daraja la baharini litakalounganisha Agha Ghan na Coco
Beach, kujenga barabara za mzunguko (Ring roads) na kununua ndege kwa ajili ya
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Pamoja na kuwapongeza
wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha bajeti
iliyowezesha kuanza kwa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa, Mhe.
Rais Magufuli amewaomba Watanzania wote kuendelea kuunga mkono juhudi hizi
kubwa na muhimu kwa maendeleo na amewataka kujiepusha na mijadala isiyo na tija
katika maendeleo.
No comments:
Post a Comment