RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA WATU MAGOMENI KOTA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, April 15, 2017

RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA WATU MAGOMENI KOTA

Ni miezi mitano sasa tangu kuanza kwa ujenzi huu. Kuaza kwa ujenzi huu ni moja ya juhudi zinazo fanywa na Serikali ya awamu ya tano, katika hili Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda  amesema  Rais pia hapa ataweka jiwe la msingi.

"Wazee  wetu waliteseka na familia zao kulikuwa na mgogoro mkubwa katika eneo hili  kwa kuwa Rais  ni msikivu alisikia kilio cha wananchi wake  na kumaliza matatizo yao. Rais Magufuli akiahidi anatimiza  na akisema ana maanisha naombeni  wanachi wote tumuunge mkono".

Kwa mujibu wa mratibu wa ujenzi huu Christina Shayo eneo hili lina jengwa nyumba za ghorofa, majengo matano yatakuwa na ghorofa  8 na  apartment 656,

Gharama ya ujenzi huu ni Bilioni 20 na unatarajiwa kukamilika kwa muda wa mwaka mmoja na  ambapo tayari miezi mitano inaelekea kuisha tangu ujenzi kuanza.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sita amesema  maamuzi yaliyo fanywa na  Rais Magufuli kumaliza mgogoro wa eneo hili na kuanza kwa ujenzi kumesaidia sana wananchi kwa kuwa waliteseka kwa  muda mrefu na kumepunguza malalamiko kwa ofisi ya Meya ambapo mwanzo watu walikuwa wanaenda ofisi hiyo kulalamika. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akiwasili eneo la ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi katika eneo la Magomeni  quotors (Kota) akiambatana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni  Benjamin Sitta, mapema jana.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akikaribishwa na waratibu wa ujenzi huo.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akitaka maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi katika eneo la Magomeni  quotors (Kota) kutoka kwa waratibu wa ujenzi huo kutoka TBA.
 RC Makonda wakwanza kushoto akipata melezo mafupi kutoka kwa wataalam waujenzi akiwa ameambatana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni  Benjamin Sitta aliyeko katikati  watatu kutoka kushoto wakwanza kutoka upande wa kulia ni mratibu wa ujenzi katika eneo hilo  Arch Christina Shayo wa TBA.
 Mratibu wa ujenzi katika eneo hilo  Arch Christina Shayo wa TBA, akitoa maelekezo kuhusu ujenzi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda alipokwenda kukagua  ujenzi wa nyumba hizo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akikagua  ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi katika eneo la Magomeni  quotors (Kota)  katika eneo hili Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mhe Paul MAKONDA akikagua baadhi ya vifaa vya  ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi katika eneo la Magomeni  quotors (Kota)  katika eneo hili Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi.
Kasi ya ujenzi ni kama inavyoonekana katika picha  kwa mujibu wa mratibu wa ujenzi huu Arch Christina Shayo  ujenzi wa ghorofa za chini unaelekea kukamilika  
 Arch Christina Shayo akitoa maelezo jinsi Mtambo wa kuchanganyia udongo (Batching Plant) kwaajili ya ujenzi ambao ni mpya unavyoweza kufanya kazi wakati RC Makonda alipotembelea na kufanya ukaguzi mapema jana. Mtambo huo umefungwa na wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao muda wowote utaanza kufanya kazi.
RC Makonda akitaka kujua jambo kuhusu mtambo wa kuchanganyia udongo (Batching Plant).
 RC Makonda  akishuka kutoka juu kukagua mtambo.
RC Makonda akitoka kukagua mtambo wa kuchanganyia udongo (Batching Plant)   kwaajili ya ujenzi ambao ni mpya, Mtambo huo umefungwa na wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao muda wowote utaanza kufanya kazi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages