Mwanamke wa miaka 22 kutoka jamii ya
kiasili Tarahumara nchini Mexico ameshinda mbio za kilomita 50 akiwa amevalia
ndala.
MarÃa Lorena RamÃrez aliwashinda wakimbiaji wengine
500 kutoka mataifa 12 katika kitengo cha wanawake huko Puebla, Mexico ya kati.
Hakuvaa mavazi yoyote ya kukimbia, na ndala zake
inaarifiwa zimetengenezwa kutoka raba ya matairi yalioharibika.
Jamii ya Tarahumara inasifika sana kwa kuwa wakimbiaji
mahiri.
Mbio hizo zimefanyika Aprili 29 lakini habari kuhusu ushindi wake zimechipuka hivi punde.
Kando na kwamba alivalia ndala lakini pia alivalia
sketi na kitambaa shingoni kukimbia katika mbio hizo. Hakupokea mafunzo yoyote
ya kukimbia.
Alishinda kwa kukimbia kwa kasi ya saa saba na dakika tatu, na alituzwa pesos 6000 ambazo ni sawa na dola 320
Taarifa zinasema kazi yake ni kuchunga ng'ombe na
mbuzi na hutembea kati ya kilomita 10- 15 kwa siku. Mwaka jana aliibuka wa pili katika mashindano ya kilomita 100
yaliofanyika huko Chihuahua.
No comments:
Post a Comment