Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha iliyokuwa ikikabiliwa na changamoto ya madarasa kujaa maji imepatiwa msaada wa kiasi cha shilingi Milioni nne na benki ya biashara ya Africa (CBA) kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya madarasa
Akikabidhi hundi katika
shule hiyo juzi Mkurugenzi wa CBA Gifti Shoko alisema kuwa lengo la msaada huo
ni kusaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya kutoa maji katika madarasa
pindi mvua zinaponyesha hali inayosababisha kukosa vipindi viwili hadi vitatu
kwa siku
Alisema kuwa msaada huo
utumike kama ulivyokusudiwa kuboresha madarasa hayo kwani ubora wa elimu
unaletwa na mazingira mazuri ya watoto kusomea
‘’Hapa nawaona Marais,
mawaziri wa kesho pamoja na wafanyakazi wazuri wa benki yetu hivyo hatuna budi
kutuoa msaada huu ikiwa kama mchango wetu wa kuboresha sekta ya elimu na
tunawahidi hatutaishia hapa tutaendelea kuwasaidia kadri ya uwezo wetu ‘’
Mwalimu mkuu wa shule
hiyo Faith Mushiro akitoa neno la shukrani alisema kuwa wanafunzi wa darasa la
tano na la sita ndiyo hasa walikuwa wakipata hadha hiyo ya kuondoa maji
madarasani pindi mvua zinapoanza kunyesha
Aidha alisema kuwa zaidi
ya vipindi viwili hadi vitatu vya asubuhi hushindwa kuhudhulia kutokana na
changamoto hiyo hivyo kupitia msaada huo wanafunzi watasoma katika vyumba
vya madarasa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma
Awali akisoma Risala
mwalimu wa shule hiyo Bw.Simon Mbawala kwa niaba ya shule hiyo alisema
kuwa pamoja na msaada waliopatiwa bado shule inakabiliwa na changamoto ya
ukosefu wa makataba ya kuhifadhi vitabu, kuharibika kwa sakafu za madarasa
pamoja na kupasuka kwa vioo vya madirisha
Hata hivyo tunatoa
shukrani zetu za dhati kwa mssada huu wa ujenzi wa vyumba vinne ambayo vilikuwa
na tatizo la kuvuja kwa maji kutokana na bati zake kuwa chakavu hali iliyokuwa
ikiwathiri sana wanafunzi na walimu hasa ikifika wakati wa kufundisha
Mkurugenzi wa Benki
ya biashara ya Africa (CBA) Gifti Shoko akikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi
Milioni nne kwa Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya
ya Arumeru Mkoani Arusha juzi Bi.Faith Mushiro kwaajili ya kukarabati madarasa
manne ambayo hujaa maji kipindi cha mvua hali ambayoilikuwa ikiwasababishia
wanafunzi kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa siku.
Mwalimu Mkuu wa Shule
ya Msingi Sing'isi Bi.Faith Mushiro akionyesha sehemu ambayo husababisha maji
kujaa ndani ya madarasa pindi mvua inaponyesha, wakatikati ni Mkurugenzi wa
Benki ya biashara ya Africa (CBA) Gifti Shoko pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo
Mwalimu Mkuu wa shule
ya msingi Sing'isi Bi.Faith Mushiro akitoa neno la shukrani kwa uongozi
wa benki ya CBA mara baada ya kupata msaada wa shilingi Millioni nne kwa ajili
ya ukarabati wa madarasa.
Mkurugenzi wa Benki
ya biashara ya Africa (CBA) Gifti Shoko akiangalia baadhi ya vifaa vya umeme
ambavyo walitoa msaada kwa shule hiyo.
Wanafunzi wakiimba
No comments:
Post a Comment