Arsene Wenger amesema hatima yake
katika klabu hiyo itaamuliwa katika mkutano wa bodi ya klabu hiyo baada ya
fainali ya Kombe la FA mnamo 27 Mei.
Mfaransa huyo wa miaka 67 amekuwa na
Gunners tangu 1996 na mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwisho wa msimu huu.
Wenger amekuwa akishutumiwa sana na
baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo, na kunao ambao wamekuwa wakiweka mabango
kumtaka ajiuzulu.
No comments:
Post a Comment