Tarehe 3 Mei, Kaimu
Balozi wa Marekani nchini Tanzania na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Virginia
Blaser alifanya ziara ya siku moja
kuwatembelea wabia mbalimbali mkoani Mwanza kuona shughuli zao akiangazia
ushirikiano imara uliopo kati ya watu wa Marekani na Watanzania katika sekta
mbalimbali.
Kaimu Balozi Blaser alianza ziara yake kwa
kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari ambayo kwa miaka miwili
iliyopita Ubalozi wa Marekani umekuwa ukiyafadhili. “ Uhuru wa habari ni muhimu
sana katika jamii ya kidemokrasia inayolinda haki za watu,” alisema Kaimu
Balozi Blaser katika hotuba yake katika maadhimisho hayo. Aidha, alisisitizia
umuhimu wa waandishi wa habari na wadau wengine wa vyombo vya habari
kushirikiana kwa kuchangia mawazo na kusaidiana kama sehemu ya mtandao mkubwa
wa kimataifa unaotoa na kuelezea mitazamo mbalimbali na kuwapa raia sauti
kuelezea kero na dukuduku zao.
Katika ziara yake katika
Taasisi ya Mafunzo ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Pasiansi, ambayo inatoa mafunzo
ya uhifadhi wa wanyamapori na kukabiliana na ujangili kwa askari wa wanyamapori
wa Kitanzania, Kaimu Balozi Blaser alishuhudia wanafunzi wakionyesha kwa
vitendo ujuzi walioupata katika usimamizi wa sheria, mbinu za medani na
historia ya viumbe asilia. Serikali ya Marekani iliichangia taasisi ya
Pasiansi kwa kufadhili mafunzo kwa wafanyakazi wake nane ili kusaidia kujenga
uwezo wa kulinda wanyamapori nchini Tanzania.
Hali kadhalika, Kaimu Balozi Blaser alipata
fursa ya kushuhudia matokeo chanya ya msaada wa Serikali ya Marekani katika
nyanja ya usalama pale alipotembelea Chuo cha Polisi Wanamaji cha Mwanza na
kuona doria ya majini inayofanywa na askari hao kwa kutumia boti maalumu ya
doria (Defender Boat) ilitolewa na Marekani chini ya Mpango wake wa Ubia na
nchi za Afrika katika kulinda Amani (African Partnership for Rapid Response
Peacekeeping). Mbali na boti mbili zilizotolewa kwa Chuo cha Polisi
Wanamaji, Marekani ilitoa boti nyingine nane kwa Tanzania na kuwezesha matunzo
na matengenezo yake.
Katika sekta ya afya, Kaimu Balozi Blaser
alizungumza na watoa huduma zinazohusu matibabu na kinga dhidi ya VVU/UKIMWI
kwa jamii wa kujitolea (Community Outreach Volunteers) ambao wamekuwa wakitoa
elimu na huduma za kujikinga na VVU kwa makundi-rika yao chini ya mpango wa
ICAP unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha Columbia. Mpango huo ni wabia wa Taasisi ya
Marekani ya Kudhibiti Maradhi (CDC) na Mpango wa Rais wa Marekani wa
Kukabiliana na UKIMWI.
Aidha alikutana na wafanyakazi wa kujitolea wa
Kimarekani kutoka Peace Corps wanaofanya kazi katika hospitali ya Bugando
wakisaidia kuimarisha utoaji wa elimu kwa matabibu na wauguzi na kuimarisha
taratibu za utoaji matibabu. Akiwa katika Kituo Maalumu cha Matibabu ya
UKIMWI kwa watoto kiitwacho Baylor International Pediatric AIDS
Initiative HIV Care Center of Excellence kilichojengwa kwa ubia kati ya
Serikali ya Marekani na Sekta binafsi nchini Marekani na kupata msaada wa
wataalamu na uendeshaji wake kupitia Shirika la Marekani la Ushirikiano wa
Kimataifa (USAID)
Kaimu Balozi Blaseraliwashukuru wafanyakazi wa
kituo hicho kwa kutoa matunzo na matibabu kwa watoto waliopata maambukizo ya
VVU na kuchangia katika jitihada za kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la
90-90-90 yaani kuhakikisha asilimia asilimia 90 ya walioathirika na maambukizi ya
VVU wanapimwa na kujua hali zao kiafya, asilimia 90 ya watakaopimwa na kukutwa
na VVU wanapata dawa za kufubaza VVU na asilimia 90 ya waliopo kwenye
tiba wawe wameweza kuvidhibiti virusi hivyo kwa kiwango kikubwa.
No comments:
Post a Comment