Jana nilikuwa nasumbuliwa na swali hilo hapo. Nilikuwa nawaza mengi sana kuhusu binadamu kulia. Nimejaribu kutafuta vyanzo nakukuta ni kama vile MAKOSA, HUZUNI, FURAHA na mengineyo ambayo hayaelezeki.
Ninajaribu kufikiria sana suala hilo ingawaje naona kwa wtoto ni jambo ambalo limekuwa katika eneo la makuzi yetu. Je nasi tunapolia tunatoa ishara kwamba hatujakua kwahiyo tunahitajika kukua?
Nawaza suala hili haya jawabu nakosa...na wakati mwingine nimewauliza wadogo au watu wazima naona jawabu lao ni moja eti kawaida. Najiuliza ingekuwaje pasingekuwepo na kulia? Nimeuliza hivi wewe Mke wako amefariki, na unajua hataweza kurejea tena kwanini unalia? Nini kinachokuliza hasa?
Wewe umemkosea mtu jambo lolote, na unajaribu kumwomba msamaha, eti huku unalia na kuangusha mchozi, kuna uhusiano gani kati ya kulia na makosa yako? Iwapo umemkosea rafikiyo, ndugu au wazazi kwanini unalia? Kuna siri gani katika kulia kwetu wanadamu?
No comments:
Post a Comment