Mageti ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid yalifungwa
kutokana na idadi kubwa ya waombolezaji huku wengine wakiendelea kuwasili.
Umati wa wakazi wa Jiji la Arusha na maeneo ya
jirani ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri
Abeid wakati wa zoezi la kuaga miili ya Wanafunzi 32, Walimu wawili na Dereva
waliopoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Rhotia Wilayani
Karatu. Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan ndie aliongonza zoezi hilo la
kuaga.
Sehemu ya Jeneza zenye miili
ya Wanafunzi 32, Walimu wawili na Dereva waliopoteza maisha kwa ajali ya
gari iliyotokea eneo la Rhotia Wilayani Karatu hivi karibuni,
zikiwa Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid wakati wa zoezi la
kuaga lililoongozwa na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya viongozi wa Vyama mbalimbali wakishiriki
kuaga miili hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa zoezi la kuaga miili ya
wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent
katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.
Jeshi la Wananchi(JWTZ) wakiingiza miili ndani ya
uwanja kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliofika
katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili hiyo.
Miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na
Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent ikiwa katika uwanja wa Shekh Amri
Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye miili ya wanafunzi
32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika
uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Samia Suluhu Hassan akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu waliofika kuaga
miili ya ndugu zao jana katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Kiserikali na
chama wakiwa kwenye uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha wakati wa
kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa
shule ya Lucky Visent.
Wanafunzi wa shule ya Lucky Visent wakiwa kwenye
majonzi wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na
Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini
Arusha.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha
wakiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa
ajili ya kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja
wa shule ya Lucky Visent waliofariki kwenye ajali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan jana tarehe 8-May-2017
ameongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani katika kuaga
miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya
Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha waliopata ajali
katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.
Katika hotuba yake kwa
wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo
pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa
na wapendwa wao.
Amehimiza wananchi kote nchini kuungana katika msiba uliotokea kwa kuwafiriji wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali peponi.
Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini, walimu, wazazi na walezi wawe makini katika kuhakikisha kuwa sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki za kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.
Amehimiza wananchi kote nchini kuungana katika msiba uliotokea kwa kuwafiriji wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali peponi.
Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini, walimu, wazazi na walezi wawe makini katika kuhakikisha kuwa sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki za kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.
Amesema hatua hiyo
itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha matukio ya ajali ambayo yanaweza kuzuilika
kote nchini.
Makamu wa Rais amewataka
madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani na waache kutumia pombe
na dawa za kulevya ili kuepukana na ajali ambazo zinagharimu maisha ya
wananchi.
Makamu wa Rais pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na Wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.
Makamu wa Rais pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na Wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.
Katika kuaga miili ya
wanafunzi, walimu na dereva katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha,
Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta amewakilishwa na Waziri wa Elimu wa
nchi hiyo Fred Matiang’i.
Ibada na Dua ya kuaga
miili hiyo, imehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali ikiwemo Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohammed Aboud, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene,
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Viongozi wa vyama vya
siasa na Viongozi wa Dini.
No comments:
Post a Comment