Mwalimu
mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia'' Kesho kila mwanafunzi aje na nyanya
kulingana na idadi ya watu anaowachukia.
Yani
kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya
mbili hivyo hivyo. Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea
madaftari na vitu vingine vya shule. Wanafunzi wakakubali, kesho yake wanafunzi
wakazibeba zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na
wengine nyingi sana.
Kama
mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi
wanawachukia.
Baada
ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu akawaambia kila mwanafunzi azirudishie
nyanya zake kwenye begi lake afu aziache humo humo ndani ya begi kila siku awe
anakuja nazo shuleni na kurudi nazo.
Baada
ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale waliobeba nyanya nyingi
kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na zinaharibu vitu vyao
,madaftari, karamu na vitu vingine vizuri walivyoweka kwenye mabegi.
Mwalimu
akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu moyoni usiowapenda.
kama
mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya kwenye begi vipi kuhusu madhara
ambayo moyo unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki dhidi ya watu.? Kwanini umchukie
mtu na kuumiza moyo wako.
Moyo
unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila wakati kila siku moyo
unakuwa na chuki na hapo.
Ndipo
unaharibika na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokuwa
moyoni, chuki uleta magonjwa ndani ya moyo, shinikizo la damu (BP), vidonda vya
tumboni, n.k
Moyo
ni kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri na Visalia.
Safisha
moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe maana ni moja ya virutubisho
vya moyo wako.
Mtu
mwenye afya njema hana chuki na wapendwa ,Ndugu zake, rafiki zake, jirani wake
. Ishi kwa furaha na upendo ili uwe na afya njema.
No comments:
Post a Comment