UMUHIMU WA KUWA NA CHAMA CHA UPINZANI KATIKA WILAYA YETU - ULANGA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, May 29, 2017

UMUHIMU WA KUWA NA CHAMA CHA UPINZANI KATIKA WILAYA YETU - ULANGA

Tangu nazaliwa hata Leo hii CCM ndio chama kinachotawala Ubunge wilayani Ulanga. Chama hiki kimefanya mambo kadhaa ambayo kwa upande fulani vimetusaidia kupata maendeleo kwa kutuletea huduma kadhaa mbalimbali vikiwamo Umeme, Benki miundombinu ya maji. Posta n.k

Lakini Chama chochote Duniani ni kama mchezo wa Mpira ili kiwe bora na kifanye vizuri kinahitaji washindani wa kweli. Huwezi ukajua uimara wa Timu yako mpaka umpate mwenye kiwango sawa cha ushindani. Mahala popote Duniani maendeleo mengi yamepatikana baada ya kuwepo kwa Ushindani wa vyama hasa kuanzia karne ya 20.

Ulanga kama wilaya nyingine MWENYE MAPENZI YA KWELI LAZIMA AKUBALIANE NA USEMI HUU YA KWAMBA WAKATI WA KULETA SIASA YA VITENDO UMEWADIA.

Naiita siasa ya vitendo kwasababu huu sasa ni wakati wa kutimiza kila Unachowaahidi wanaUlanga na hilo litawezekana IKIWA ULANGA UTAKARIBISHA UPINZANI ILI KUWAAMSHA WALIOPO MADARAKANI NA KUWAKUMBUSHA KUWA SASA NI WAKATI WA KUISUKA ULANGA MPYA.

Wilaya nyingine zilizoendelea kwa sasa na zinazokuja juu kimaendeleo nyingi sana Zinawapinzani Imara mfano kidogo tu Kigoma kaskazini chini ya Zitto Kabwe. Wilaya za mkoa wa Urusha na Kusini kwa Nchi zetu. Miaka ya chini ya 2000-1990s kusini mwa nchi kunausemi unasema kulisahaulika yaani kulikuwa nyuma kimaendeleo ukifananisha na mikoa ya kati, kaskazini, kaskazini mashariki.

Lakini Ukiongelea Kusini ya sasa unazungumzia Mikoa tegemezi kiuchumi ya kesho sio eti kwasababu ya gesi iliyogunduliwa tu hapana Bali kutokana na UPINZANI has a CUF kuingia na kuleta mapinduzi makubwa kiutawala hata sasa ukienda mikoa ya Kusini kama unaenda Dodoma tu.

Mfano ukitoka Dar kuja ULANGA na atakayetoka Dar es laam kwenda Mtwara ataanza kufika mtwara au mkafika sawa na MTU anayetembea ndani ya mkoa wake kwasababu kutoka Dar es Salaam utapita pwani na kuingia Moro mjini SAA 4 asubuhi sasa kutokana pale mpka Mikumi kama Km 60 - 70 kama sijakosea utafika SAA 6-7 lakini cha ajabu kutoka Mikumi mpaka Ulanga ndani ya wilaya mbili unatembea kwa masaa 5-6 lakini kutoka Dar mpaka Moro unapita mikoa mitatu unatumia Masaa manne hii sio vyema.

Wapendwa Barabara ndio uti wa mgongo wa maendeleo kwa Dunia ya Leo.Hakuna mahali palipopiga hatua kimaendeleo penye miundombinu mibovu.

Mtwara imejengwa kwa jasho la wanamtwara Urusha imejengwa na waarusha na kigoma imejengwa na wanakigoma wenyewe waliweka Uzalendo wa kwao kwanza walifanikiwa.

Muda umefika wa kuamka na kuweka mapenzi ya dhati ya ujenzi wa Wilaya yetu. Upendo wa chama uwepo lakini wilaya kwanza maana kama chama kinajenga nahisi Ulanga ingekuwa mji.

Tumechoka kutukanwa na kutaniwa na marafiki zetu kuwa tunachagua viongozi wachekeshaji. Chozi la Ulanga linatiririkia mikononi mwako likilia kwa uchungu wa hali yake na we we ni doctor mmwenye mwarobaini kichwani kwako.

Amka Tuijenge Ulanga chozi hili kwangu kama mkuki wa moto uliochomwa moyoni na kupata maumivu ya aina mbili:

            1.    Maumivu ya kutobolewa kwa nyama ya mwili mpaka moyo wilaya kupoteza, kukosa zao maalumu la biashara kumbuka kilimo ni uti wa mgongo katika nchi yetu hivyo unapoanguka kwenye kilimo sawa na mtu mapigo ya moyo kusimama au sawa na gari kuzima injini ilihali IPO safarini tena katikati ya msitu wenye wanyama wakali huku limejaza watu

             2.    Maumivu ya moto.

Wilaya kuwa na miundombinu mibovu hill sawa na kupakata kaa la moto ilihali unawaka kwa walio ndani ya Ulanga ni vigumu kuelewa coz wao kukarabatiwa barabara ya vumbi na kupita vinoa basis wameridhika sisi tulio nje ya wilaya tuajua tukisemacho). Hivyo ili kupoza maumivu haya tunahitaji kuungana Tuamke sisi kisha tukawaamshe wengine ili tuweze kuijenga Ulanga tuachane na imani potofu tunazopitishwa na maakida Fulani wakisema Ukichagua UPINZANI huletewi maendeleo tuwajibu kuwa maendeleo sio gari sema Ulikokote kulileta mahali wala maendeleo sio Umeme Sena uuvute tu Bali maendeleo huletwa na Mwananchi wenyewe tena mmoja mmoja. Kwa pamoja tunaibadilisha wilaya yetu.


Kwakutumia jukwaa hili ningependa kuikumbusha Serikali ya chama tawala kuliangalia hili kwa makini tofauti na hivyo, wananchi watafikia ukomo wa uvumilivu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages