Suala
la uhaba wa vitabu vya masomo ya Sayansi, maabara pamoja na walimu wa masomo
hayo limekuwa likisababisha baadhi ya wananfunzi kushindwa kumudu na hivyo
kuyaepuka masomo hayo,licha ya serikali na wadau mbalimbali kuhamasisha
wanafunzi kuchukua masomo hayo.
Kutokana
na hali hiyo Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel imetoa msaada wa Vitabu vya
Masomo ya Sayansi vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu katika Shule ya
Sekondari Vianzi iliyopo Mkuranga Mkoani Pwani
ambayo ina zaidi ya wanafunzi 400 ikiwa na walimu watatu kwa masomo yote ya
Sayansi (biolojia, fizikia, kemia na hesabu). Hatua hiyo ni mwendelezo wa
Kampuni hiyo kusaidia katika elimu shule mbalimbali hapa nchini ili kuinua
kiwango cha elimu katika masomo ya Sayansi.
Mkuu wa shule ya Shule ya sekondari ya Vianzi
Ashura Manaki ( wa pili kulia ) akifuatiwa na pamoja na Meneja Huduma kwa Jamii
wa Airtel, Bi Hawa Bayumi (wapili kushoto) na Meneja Mauzo wa Airtel Pwani,
Philipi Nkupuma kwa pamoja wakionyesha vitabu vya sayansi mara baada ya Airtel
kukabidhi vitabu hivyo kwa shule ya sekondari ya Vianzi pindi walipotembelea
shuleni hapo.
Mkuu wa Shule ya
Sekondari Vianzi Mwl. Ashura Manaki amesema kuwa shule yake imekuwa ikikabiliwa
na changamoto ya ukosefu wa walimu, maabara za kutosha pamoja na vitabu hali
ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi kukimbia masomo ya Sayansi.
“Tunaishukuru
sana Airtel kwa msaada huu wa vitabu ebu fikilia tuna upungufu wa walimu,sasa
likija tatizo la ukosefu wa vitabu unadhani wanafunzi watayapenda masomo ya
sayansi,lakini kwa sasa nina matumaini tutaweza kusonga mbele,”alisema Manaki.
Kwa upande wa Meneja wa
Huduma kwa Jamii kutoka Airtel Hawa Bayumi ameleeza kuwa licha ya Kampuni hiyo
kujikita katika mambo mbalimbali ya Kijamii wameona umuhimu wa kuisaidia shule
hiyo ambayo inachangamoto ya walimu wa sayansi lakini wakakuta hata vitabu
navyo ni changamoto wakaamua kutoa msaadahuo.
”Licha
ya Airtel kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii tumeona kuna umuhimu mkubwa
kuisaidia vitabu vya sayansi shule hii kutokana na kukabiliwa na changamoto ya
uhaba wa walimu wa sayansi pamoja na vitabu vya sayansi tuna matumaini vitaweza
kusaidia shule hii kujenga wataalamu wa sayansi hasa ukizingatia serikali
inaweka juhudi kufikia Tanzania ya viwanda ni muhimu kuwekeza katika rasilimali
watu na kujenga watanzania weny weledi. Lengo letu ni kuendelea kuwezesha
vijana kufikia malengo yao kupitie elimu na ujasiriamali,”alisema Bayumi.
Zamda Said ni Mwenyekiti
wa Bodi ya Shule hiyo amesema kuwa shule hiyo bado ina mahitaji ya walimu wa
sayansi lakini kwa kupatiwa vitabu hivyo vitasadia hata wanafunzi kuweza
kujisomea huku akiwaasa wanafunzi kutumia fursa hiyo kufaulu masomo ya sayansi.
“Ni
kweli tatizo la uhaba wa walimu pamoja na ukosefu wa vifaa vya kujifunzia na
kufundishia ni changamoto kwa shule hii lakini nawaombeni wanafunzi kutumia
fursa hii kuweza kujisomea maana vitabu gharama yake ni kubwa,”alisema Said.
Meneja Huduma kwa
Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi akimkabidhi vitabu vya sayansi, Maria Edward,
mwanafunzi wa Shule ya sekondari ya Vianzi iliyopo Mkuranga wakati Airtel
ilipotembelea shule hiyo kutoa msaada wa vitabu vya taaluma .
Meneja Huduma kwa
Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi akimkabidhi vitabu vya sayansi mwalimu mkuu wa
shule ya sekondari ya Vianzi Bi Ashura Manaki wakati Airtel ilipotembelea shule
hiyo kutoa msaada wa vitabu vya taaluma, akishuhudia ni Zamda Said ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule.
No comments:
Post a Comment