Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Josephat Gwajima amefunguka na kusema Watanzania tumerogwa kwani tuna kila kitu
ambacho kinaweza kutufanya kuwa mbele kimaendeleo lakini siku zote tumekuwa
nyuma.
Askofu wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
Mchungaji Gwajima amesema hayo jana wakati akitoa mahubiri
yake kwenye kanisa lake na kusema Watanzania wamerogwa kwani wanapenda sana
maandamano na vitu visivyo na msingi kuliko kufanya kazi, anasema Tanzania ina vitu
na mali nyingi.
"Ukitaka kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa
mwendawazimu maana watu wake wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka
tu unaweza kwenda kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa madini
Japan au Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na karanga mzungu
anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito mingi yenye maji lakini
maji yanakwenda tu, watu hawalimi" alisema Gwajima.
Mbali na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa
kitendo chake cha kuzuia makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais
ashikirie hapo hapo.
"Hata kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu
Rais ashikirie hapo hapo hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe
mekundu, kama hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema
sijui tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa
yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe madini hakuna
kwenda" alisema
Gwajima.
No comments:
Post a Comment