• Yapata faida ya shilingi bilioni 40.9 kwa
miezi Mitatu
• Ni ongezeko la
asilimia 4
BENKI ya NMB imepatafaida
ya shilingi Bilioni 40.9 kwa miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka ikiwa ni ongezeko
la 4% ya faida ukilinganisha na kipindi kama hicho Mwaka jana – 2016 ambapo NMB
ilipata faida ya shilingi Bilioni 39.3. Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Ineke Bussemaker
alisema mwanzo huu wa Mwaka mzuri katika faida ya benki umetokana na kuimarika
kwa pato linalotokana na biashara ya benki na ahueni iliyopatikana katika
mikopo mibovu au isiyolipika.
Bi Bussemaker alisema
pato linalotokana na biashara ya benki lilikua kwa asilimia 4.6 hadi kufikia
kiasi cha shilingi bilioni 58.7 ikilinganishwa na kiasi cha bilioni 56.1
zilizopatikana katika kipindi kama hicho mwaka jana.
Mkurugenzi wa Benki ya
NMB - Ineke Bussemaker
Alisema ongezeko hili
limechangiwa kwa kiasi kikubwa na pato linalotokana na riba katika mikopo na
biashara ya fedha za kigeni ambalo limeongezeka kwa asilimia 41 hadi kufikia
kiasi cha shilingi bilioni 4.9 katika robo ya kwanza ya mwaka huu
ikilinganishwa na shilingi bilioni 3.5 zilizopatikana katika kipindi kama hicho
mwaka jana.
“Robo ya kwanza ya mwaka
2017, pato linalotokana na riba katika mikopo ilikuwa shilingi za kitanzania
bilioni 115.9, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.4 ikilinganishwa na kiasi cha
shilingi bilioni106.0 katika kipindi kama hicho mwaka jana na pia
ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.9 hadi shilingi bilioni 114.9 katika
robo ya mwisho ya mwaka 2016,” alisema Bi Bussemaker.
Pia taarifa hii ya hesabu
za benki inaonyesha kuwa pato lisilotokana na riba katika mikopo limeongezeka
kwa asilimia 5.3 hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 41.5 katika robo ya
kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni 39.4 katika
kipindi kama hicho mwaka jana na pia ikilinganishwa na ongezeko la asilimia nne
kutoka shilingi bilioni 39.9 katika robo ya nne ya mwaka 2016.
Amana za wateja nazo
ziliongezeka kwa asilimia 0.9 hadi kufikia shilingi trilioni 3.75 katika robo
ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.71 katika robo ya
mwisho ya mwaka jana. “Ili kuongeza idadi ya wateja na amana, benki imeweza
kutumia zaidi NMB wakala, walioponchi nzima. Lengo la benki ni kuwa na mawakala
wapatao 4,500 mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu," alisema Bi
Bussemaker
Bi Bussemaker pia alisema
katika kupambana na changamoto ya ukata katika soko, benki imeweza kuongeza
umakini katika kutoa mikopo kwa Wateja. Mikopo iliyotolewa kwa Wateja katika
robo ya kwanza yam waka ilipungua kwa 1.2% mpaka kufikia shilingi trilioni 2.76
kutoka shilingi trilioni 2.79 zilizonukuliwa katika robo iliyopita. Uwiano wa
mikopo na amana za NMB umeendelea kuwa mzuri kwa Kiwango cha 74.6%, ukusanyaji
wa mikopo inadhihirishwa na Kiwango cha mikopo mibaya au isiyolipika ambacho
kimepungua mpaka kufikia 4.6% kutoka 4.8% iliyopatikana mwaka jana.
“Menejimenti imedhamiria
kuendelea kutoa hesabu nzuri na mwisho wa siku kuleta matunda kwa wana hisa wa
benki ya NMB kwa mwaka 2017,” alisema Bi Bussemaker. Kuhusu NMB: NMB ni benki
inayoongoza nchini Tanzania kwa matawi, ikiwa na zaidi ya matawi 189, wateja
zaidi ya milioni 2 na laki tano na zaidi ya mashine 700 za kutolea fedha (ATM)
nchi nzima.
NMB imeasisi ubunifu
mkubwa katika soko la Tanzania ikiwa ni pamoja na huduma za benki kwa njia ya
simu yaani NMB mobile, Pesa Fasta na malipo kwa kutumia mashine za ATM. NMB
inaendelea kujikita katika kutoa huduma kwa makampuni makubwa, masoko ya
kifedha pamoja na huduma za kusaidia makusanyo ya kifedha na biashara. Lakini
Pia imekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya kilimo na imeanzisha mfumo wa
stakabadhi ghalani kupitia vyama vya ushirika nchini.
No comments:
Post a Comment