Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack
akifungua mkutano wa wadau wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa
vyombo vya habari duniani ngazi ya mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,
Kadama Malunde akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa habari mkoa wa
Shinyanga kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani Mei 3, 2017
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,
Kadama Malunde akitoa hotuba ukumbini
Wadau wa habari wakiwa ukumbini
Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga, Stephen Wang'anyi akisisitiza jambo ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Mwandishi wa habari Suleiman Shagata akichangia
hoja ukumbini
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde akiongoza majadiliano ukumbini
Kaimu Mwenyeti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Shaaban Alley akizungumza ukumbini
Mratibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga, Nunu Abdul akiandika dondoo muhimu
Wadau wakiwa ukumbini
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Mkutano unaendelea
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP
Muliro Jumanne Muliro akizungumza ukumbini
Msaidizi wa Askofu Kanisa kuu la KKKT Shinyanga
Usharika wa Ebenezer Trafaina Assery Nkya akizungumza ukumbini.
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire
akizungumza ukumbini
Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani
akizungumza ukumbini
Kanali Mussa Kingai ambaye ni mwakilishi wa vikosi
JWTZ Shinyanga kwenye kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga akichangia
hoja ukumbini
Mdau Gelard Ng'ong'a kutoka shirika la Rafiki SDO
akichangia jambo
Afisa habari kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira
Mji wa Kahama (KUWASA) Bwana Mkama akichangia hoja
Mdau wa habari Bwana Chief Abdallah Sube akichangia
hoja
Bwana John Myola kutoka Shirika la AGAPE Shinyanga
akizungumza ukumbini
Mkurugenzi Msaidizi Radio Faraja, Bwana Anikazi
Kumbemba akizungumza ukumbini
Mwakilishi wa Kamanda
wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga, Bi Alice Mazoko akichangia hoja
Mwandishi wa habari Patrick Mabula akifuatilia
kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack
akizungumza ukumbini
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga
mheshimiwa Zainab Telack,wadau wa habari na waandishi wa habari.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga
mheshimiwa Zainab Telack, wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa
Shinyanga na waandishi wa habari.
Katika kuadhimisha siku
ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC), leo Mei 3, 2017 imefanya mkutano na wadau
wa habari mkoani Shinyanga kujadili namna klabu hiyo ilivyo na wajibu wa
kuendeleza amani katika jamii.
Mgeni rasmi katika
mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel mjini Shinyanga alikuwa
mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack aliyekuwa ameambatana na
baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga.
Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari huadhimishwa duniani kote kila ifikapo tarehe 3 mwezi Mei ya kila
mwaka ambapo pamoja na maadhimisho ya kitaifa kufanyika kitaifa jijini
Mwanza, lakini yamefanyika pia katika kila mkoa nchini yakiwa na kauli mbiu
inayosemayo “Klabu za Waandishi wa Habari zina wajibu wa kuendeleza amani
katika jamii”.
Awali akitoa hotuba yake,
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde alisema
Klabu za waandishi wa habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii hivyo
kuwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao vizuri kuandika habari
zinazojenga utaifa na kuleta mshikamano katika jamii.
Malunde alisema Klabu za
waandishi zinawaweka pamoja waandishi wa habari hivyo kupitia umoja huo
zinawabijika kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza amani katika jamii kwani
pasipo na amani hakuna maendeleo.
Aliongeza kuwa kutokana
na nguvu ya vyombo vya habari, amani katika jamii itaendelea kuwepo endapo tu
waandishi wa habari watazingatia maadili ya kazi yao na kuepuka kushabikia
mambo yasiyo na maana.
Kwa upande wake mkuu wa
mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack aliwataka waandishi wa habari
kutanguliza utanzania na uzalendo katika habari wanazoandika.
“Ndugu zangu waandishi wa
habari mnajukumu kubwa la kulinda amani ya nchi hii, tumieni kalamu zenu
vizuri, epukeni kuandika habari za kujenga hofu na mnapoandika basi msiegemee
upande mmoja, sikilizeni hata upande wa pili ili kutenda haki”, alieleza mkuu wa
mkoa.
Katika hatua nyingine
Telack aliwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha mshikamano walionao na
kujiendeleza kielimu huku akiwashauri kuanzisha miradi itayowakomboa kiuchumi
kwani fursa mbalimbali za kiuchumi zipo mkoani humo.
“Nitoe wito kwa waandishi
wa habari kuunga mkono sera ya uchumi wa viwanda, andikeni habari kuhusu viwanda
na kilimo na kupitia umoja wenu anzisheni mashamba ya pamba na alizeti na mnao
uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo ili kuinua uchumi wenu, andikeni proposal
mnaweza kuanzisha hata kiwanda cha maziwa”, aliongeza Telack.
No comments:
Post a Comment